KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA SHILELA CHAADHIMISHA SIKU 16 ZA KUPINGA UKATILI WA KIJINSIA, WANAWAKE WALIA MFUMO DUME

 Mwenyekiti wa kikundi cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Rahab Nkwabi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Na Marco Maduhu, KAHAMA

KITUO cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama, kime adhimishia siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, huku tatizo la mfumo dume likipingwa kila kona ili kuwapa wanawake fursa ya kumiliki mali.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Desemba 6,2022 katika kijiji cha Nyikoboko Kata ya Shilela, huku Mgeni Rasmi akiwa ni Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Msalala Richard Ng'ondya.

Mwenyekiti wa kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela Rahabu Nkwabi, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, amewataka wanawake na watoto kupaza sauti juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia ili watatuliwe matatizo yao na kuishi kwa amani.

Amesema wanawake wengi kwenye Kata hiyo wamekuwa wakifanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia, lakini hawatoi taarifa huku akiwapongeza wale ambao wanapaza sauti na kutatuliwa matatizo yao ikiwamo manyanyaso yanayotokana na mifumo dume ambayo hukandamiza wanawake na kuwazuia kumiliki mali.

"Nawaombeni sana wanawake na watoto toeni taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia, ambavyo huwa mnafanyiwa, msikae kimya na kuendelea kuumia, sisi kituo cha Taarifa na Maarifa tupo kwa ajili ya kupinga vitendo hivi vya ukatili," amesema Nkwabi.

"Nampongeza mama mmoja mjane ambaye hivi karibuni amekuja kwetu na kutupatia taarifa juu ya unyanyasaji ambao anafanyiwa na Shemeji yake, baada ya mume wake kufariki dunia na kutaka kunyang'anywa mashamba aliyoachiwa na mume wake na sisi tutakuwa naye bega kwa bega ili kumsaidia na kupata haki yake," ameongeza.

Naye Mwanamke huyo Njiku Dome ambaye ana watoto watano, amesema mara baada ya mume wake kufariki dunia mwaka jana (2021), ukoo mwanaume ulikaa na kumuachia mashamba hayo ili aendeleze kuyalima na kuwalea watoto wake, lakini cha ajabu Shemeji yake ameanza kumsumbua kuyataka mashamba huku akitishia pia kuwachukua na watoto.

Aidha, ameiomba Serikali pamoja na wanaharakati wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wamsaidie kupata haki yake na kunufaika na mali ambazo alizichuma na mume wake akiwa bado hai, ili awalee watoto wake na kuwapatia elimu.

Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Msalala Richard Ng'ondya, amekemea vitendo vya wanaume kuendekeza masuala ya mfumo dume na kuwakandamiza wanawake wasimiliki mali na kusema hizo mila zimeshapitwa na wakati, ambapo kwa sasa wanawake wanapaswa kujengwa kiuchumi.

Amesema mwanamke akimiliki mali na kuwa vizuri kiuchumi, atahudumia vizuri watoto wake na hawataweza kuteseka, tofauti na wanaume ambao wenyewe wakipata fedha baadhi yao huendekeza mambo ya anasa na mwisho wa siku wanatelekeza familia.

Mtendaji wa Kata ya Shilela Mwanaidi Mzee, amewataka wananchi wasisite kutoa taarifa za matukio ya ukatili ili wapate kusaidiwa kabla ya madhara kutokea, huku akiahidi kulishughulikia suala la Mwanamke Mjane ambaye anataka kunyang'anywa mashamba na Shemeji yake.

Vituo vya Taarifa na Maarifa vilianzishwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kwa lengo la kuleta ukombozi wa kimapinduzi dhidi ya wanawake na watoto katika kupata haki zao.

Maadhimisho hayo ya kupinga ukatili wa kijinsia yatafikia tamati Desemba 10,2022.

Mwenyekiti wa kikundi cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Rahab Nkwabi akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Katibu wa kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama Joseph Samweli akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Rhoda Gervace Afisa Tathimini na Ufuatiliaji kutoka kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala wilayani Kahama akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Afisa Ustawi wa Jamii Halmashauri ya Msalala Richard Ng'ondya akizungumza kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, katika Kata ya Shilela maadhimisho yaliyoandaliwa na kituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela.

Mtendaji wa Kata ya Shilela Mwanaiddi Mzee akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mwenyekiti wa kijiji cha Nyikoboko Kata ya Shilela John Sengerema, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Mama Mjane Njiku Dome akieleza namna anavyofanyiwa ukatili wa kijinsia na Shemeji yake kwa madai ya kutaka kumnyang'anya mashamba aliyoachiwa na mumuweka ambaye kwa sasa ni marehemu.

Wanakituo cha Taarifa na Maarifa Kata ya Shilela wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakiendelea katika Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakiendelea Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala.

Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakiendelea Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala.

Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia yakiendelea Kata ya Shilela Halmashauri ya Msalala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments