SHIRIKA LA TCRS LAENDESHA MAFUNZO YA STADI ZA MAISHA KWA WASICHANA BALEHE, AKINA MAMA VIJANA NA WENYE ULEMAVU KISHAPU


Watetezi wa haki za Binadamu na wadau wa maendeleo ya jamii Mkoani Shinyanga likiwemo shirika lisilo lakiserikali linalojihusisha na utoaji wa misaada ya kibinadamu na utunzaji wa mazingira la TCRS wameunga mkono juhudi za Serikali kupinga ukatili wakijinsia kwa kutoa elimu ya stadi za maisha kwa wasichana balehe,wanawake vijana na watu wenye ulemavu walioathirika na vitendo vya ukatili kupitia mradi ujulikanao kama CHAGUO LANGU - HAKI YANGU unaofadhiliwa na Serikali ya Finland kwa kushirikiana na UNFPA na kutekelezwa na TCRS na WILDAF.


Mratibu wa miradi ya TCRS Kellen Machibya amesema mradi huo unashirikisha makundi matatu ya wasichana kuanzia umri wa miaka 10 hadi 19 ambayo ni wasichana balehe, wanawake vijana na wasichana wenye ulemavu ambapo ameeleza kuwa malengo makuu ni kuwafundisha stadi za maisha ili waweze kuishi kama watu wengine na kujiepusha na vishawishi vinavyosababisha vitendo vya ukatili.


Baadhi ya walengwa wa mradi huo wamesema awali walikuwa hawavijui vitendo vya ukatili ni nini hali iliyowasababishia kufanyiwa ukatili bila kujua na kupata madhara lakini baada ya kupata elimu ya stadi za maisha itawasaidia kuishi maisha ya kawaida na kujiepusha na vishawishi vinavyoweza kusababisha wafanyiwe ukatili.


Mariam Lyiuba ni mmoja kati ya mabinti walionusurika kuozeshwa akiwa na umri mdogo amesema baada ya kupata elimu hiyo yeye na wenzake wako tayari kueneza elimu hiyo kwa mabinti na wanawake wengine ili jamii iondokane na changamoto ya vitendo vya ukatili na unyanyasaji wakijinsia.


Mratibu wa mradi wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU kata ya Maganzo wilaya ya Kishapu Regina Hipolit amesema makundi hayo matatu yaliyotajwa ni waathirika wakubwa wa vitendo vya ukatili lakini elimu hiyo imelenga kuwakomboa kiuchumi kwakuwa wanafundishwa mabo ya lishe, afya ya uzazi pamoja na kujikinga na ukatili wakijinsia ambapo vijana hao walikuwa hawana uelewa juu ya mambo hayo na elimu hiyo itawasaidia kujua haki zao kwenye maisha.


Mwezeshaji wa mafunzo ya stadi za maisha kupitia MRADI WA CHAGUO LANGU HAKI YANGU Bi. Vestina Mtakyawa amesema tatizo kubwa linalowapata babinti wanaopata mimba za utotoni ni kushindwa kuwalea watoto na kusababisha changamoto ya utapiamulo, magonjwa mbalimbali, na ongezeko la watoto wa mitaani lakini kwa kupata elimu hiyo mimba za utotoni zitapungua lakini pia vifo vya wanawake wajawazito na watoto wachanga vitapungua.


Afisa maendeleo ya jamii kata ya Maganzo Neema Gweso amesema mabinti balehe na wanawake vijana ni kundi linaloathirika zaidi na vitendio vya ukatili wakijinsia katika jamii na ukatili ulioshamiri zaidi ni mabinti kuozeshwa wakiwa na umri mdogo, kuwaogesha dawa ya mvuto wa mapenzi ijulikanayo kama samba sababu kuu ni wazazi kutafuta utajiri wa haraka.


Fatuma Katabaro ni msaidizi wa kisheria kutoka Kishapu Para-legal Organization amesema kupitia mradi huo wa CHAGUO LANGU HAKI YANGU kesi nyingi za ukatili zinazofikishwa kwao zitapungua kwakuwa hali ya ukatili wa kijinsia kabla ya hapo ilikuwa ni kubwa changamoto mtambuka ikiwa ni jamii kutotambua kuwa mtoto ni nani.

Afisa ustawi wa jamii mkoa wa Shinyanga Lydia Lwesigabo amesema vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia bado vinaendelea kushamiri mkoani humo huku akivitaja kuwa ni ukatili wa kingono, ulawiti,ubakaji na utelekezaji wa watoto na vipigo mila na kutaja mila na desturi potovu kuwa chanzo mtambuka kwa ukatili.

Ametaja sababu zinazochangia vitendo vya ukatili wa kijinsia ni pamoja na tamaa, umaskini wa kipato na mila zilizopitwa na wakati mfano kuozesha watoto wa kike.

Aidha amesema serikali inashirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo TCRS na vyombo vya habari kupitia mradi wa chaguo langu haki yangu wa TCRS wakiongozwa na mpango mkakati wa kutokomeza ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watiotoi (MTAKUWWA).
Mratibu wa Miradi TCRS, Kellen Machibya akizungumza
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akizungumza
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akizungumza
Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Shinyanga Lydia Kwesigabo akizungumza
Mratibu wa Mradi wa Chaguo Langu Haki Yangu Maganzo wilayani Kishapu, Regina Hipolit akizungumza

Mwezeshaji wa mafunzo Vestina Mtakyawa akizungumza
Mwezeshaji wa mafunzo Vestina Mtakyawa akizungumza


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments