MAZISHI YA WAKALA WA FEDHA ALIYEUAWA KWA KUPIGWA RISASI NA WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI YAFANYIKA MASABI MSALALA



Waombolezaji wakishiriki mazishi ya Richard Nzumbe.

*****
Mazishi ya mwili wa Wakala wa Fedha Richard Nzumbi aliyeuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodaiwa kuwa majambazi Mjini Shinyanga yamefanyika Desemba 22, 2022 nyumbani kwao katika 
kijiji cha Masabi kata ya Mega Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.

Akizungumza kwa niaba ya Mawakala wa Fedha,Danford Masawe amesema msiba umewaachia majonzi makubwa huku akiiomba serikali kuwawekea ulinzi shirikishi kulingana na biashara zao kuwa hatarini.


Aidha ameliomba Jeshi la polisi kutofumbia macho tukio hilo sambamba na kutoa adhabu kali kwa watakaobainika kuhusika na na tukio hilo.

Richard Nzumbe alizaliwa mwaka 1988 katika kijiji cha Masabi ambapo alifikwa na umauti Desemba 20,2022 na ameacha watoto watatu wa kike na mjane mmoja ambaye ni mjamzito.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments