MKUU WA WILAYA AHUKUMIWA KULIPA MILIONI 80 KWA KUMDHALILISHA MWANANCHI TABORA

 

Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Tabora leo imemuhukumu aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Tabora mjini KOMANYA KITWALA kumlipa fidia ya kiasi cha shilingi Milioni 80 kwa ALEXANDER NTONGE mkazi wa kata ya Ipuli Tabora mjini baada ya kupatikana na hatia katika mashitaka aliyofunguliwa ya kuwaamuru askari Polisi kumkamata  na kumdhalilisha isivyo halali.


Akisoma hukumu hiyo katika shauri la madai namba 4 la mwaka 2021,hakimu mkazi JOVITH KATO alisema mahakama imepitia ushahidi wa pande zote mbili na kujiridhisha kwamba KOMANYA KITWALA alitenda kosa hilo  Januari 5 mwaka 2020 na hivyo mahakama imemuhukumu kulipa kiasi hicho cha fedha Milion 80 badala ya shilingi Milion 140 ambazo mlalamikaji ALEXANDER NTONGE alizodai kulipwa kutokana na makosa ya udhalilishaji aliyofanyiwa na KOMANYA KITWALA wakati alipokuwa mkuu wa wilaya ya Tabora mjini.


Awali wakili wa mlalamikaji KELVIN KAYAGA aliiambia mahakama KOMANYA KITWALA alikwenda nyumbani kwa mlalamikaji akiwa na askari Polisi ambao aliwaamuru kumkamata na kumtesa kisha kumuweka ndani katika Kituo Kikubwa cha Polisi Tabora mjini bila kuwa na kosa lolote ambapo baadae aliyekuwa kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora kwa wakati huo ACP SAFIA JONGO aliagiza mlalamikaji ALEXANDER NTONGE kuachiliwa huru kwa madai kulikuwa hakuna kosa lolote lililofanya kukamatwa na kuwekwa ndani jambo ambalo lilionekana ni udhalilishaji wa waziwazi uliokuwa umefanywa na kiongozi huyo wa Serikali ya wilaya kwa wakati huo.

Chanzo - Tabora Press Club

https://www.instagram.com/p/Cmy2YqFqeHa/?igshid=MDJmNzVkMjY=

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments