MKE AMKATA PANGA MMEWE KISA KAKOSA PESA YA KUSUKIA NYWELE ZA KRISMASI

Hazraj Latif Byakika (kushoto) ambaye alishambuliwa na mke wake kwa panga. Picha: New Vision 

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 23 anauguza majeraha mabaya kichwani baada ya kukatwa panga na mke wake kufuatia mzozo wa nyumbani.

Hazraj Latif Byakika raia wa Uganda anaripotiwa kushambuliwa na mke wake Fauzi Namuli mnamo Ijumaa - Disemba 23 - baada ya kushindwa kupata hela za kumpa asuke nywele zake kwa ajili ya sherehe za Krismasi.

Gazeti la New Vision linaripoti kuwa Fauzi alimshambulia mume wake akimkata vibaya kichwani kwa kutumia panga.

 Mwanamume huyo alipiga kamsa akiitisha msaada na majirani walipofika, walimkuta akihema na chirizi la damu likitoka kichwani kwake.

Latif akimbizwa hospitalini akitokwa na michirizi ya damu Latif alikimbizwa katika kituo cha afya cha Kakooge nchini humo kwa huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa katika Hospitali ya Kamuli kwa matibabu zaidi.

 Akizungumza na waandishi wa habari baada ya hali yake kudhibitiwa, Latif alisema kuwa mke wake alianza kuagiza pesa za kusuka nywele zake wiki mbili zilizopita.

Aliahidi kumpatia pesa hizo kabla ya siku ya Krismasi - Disemba 25,2022  lakini hilo halikutimia kutokana na ugumu wa kifedha anaopitia kwa sasa. 

Fauzi atoweka Kufuatia kisa hicho.

Fauzi alitoweka na kwa sasa anasakwa ili kujibu mashtaka ya jaribio la mauaji na kumsababishia mwenzake majeraha ya mwili.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments