WAZIRI NAPE : HAKUTAKUWA NA MABADILIKO YA BEI ZA BANDO MPAKA TATHIMINI YA GHARAMA ZA BANDO UTAKAPOKAMILIKA

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 21,2022 katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 21,2022 katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Jijini Dar es Salaam.

*****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

IKIWA Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha inatoa unafuu wa bei za bando kwa wananchi kwa kugfanya tathimini ya gharama za bando hakutakuwa na mabadiliko ya bei hizo mpaka zoezi hilo litakapokamilika.

Ameyasema hayo leo Novemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe.Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Amesema tathimini hiyo inatarajiwa kukamilika kati ya mwezi Desemba 2022 hadi mwezi Januari 2023.

Aidha Waziri Nape amesema kuwa kwa sasa watoa huduma wote wako katika viwango vya bei eekezi iliyowekwa na Serikali ambayo ni kati ya Sh2.03 hadi Sh9.35.

"Sasa tumefikia hatua ambayo tumesema tutatulia hadi tathmini itakapokamilika na matumaini yetu kuwa itatupa muelekeo mzuri". Amesema Waziri Nape.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

1/Post a Comment/Comments

  1. Kiukweli sijawahi ridhishwa na utendaji wa huyu kijana kabisa. Anamaneno mengi lakini utekelezaji hakuna. Hata hoja zake nyingi kwangu mimi huwa hazina mashiko.

    ردحذف

إرسال تعليق