MAHAFALI YA KWANZA CHUO CHA VETA 'ShyNet' YAFANA SHINYANGA

Mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto akigawa vyeti kwa mhitimu
Mkuu wa chuo cha ShyNet Abubakar Rehani pamoja na mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto wakiangalia Nguo zilizoshonwa na wahitimu wa fani ya Ushonaji.

Na Mwandishi Wetu - Malunde 1 blog

CHUO cha Shinyanga Network Training Center (ShyNet ) kilichopo katika Kata ya Lubaga Mkoani Shinyanga, kimefanya mahafali ya 1 chuoni hapo, kwa kuwaaga wahitimu wa mwaka wa pili kutoka fani mbalimbali.

Mahafali hayo yamefanyika chuoni hapo Novemba 17,2022, na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali ,na Taasisi binafsi huku mgeni rasmi akiwa ni Diwani wa kata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Reuben Dotto.

Akizungumza kwenye Mahafali hayo Mkuu wa chuo cha ShyNet  Shinyanga Abubakar Rehani, amesema chuo hicho kilianzishwa mwezi January mwaka 2021,na kuanza kutoa fani 2 ambazo ni fani ya ufundi Umeme ,Ushonaji na ubunifu wa mavazi , lakini mpaka sasa chuo kinatoa kozi za muda mrefu na mfupi.

Amesema chuo kilianza kikiwa na mwanafunzi mmoja lakini wamehitimu wanafunzi 12 wa kiume wakiwa 7 na wa kike 5, na kubainisha kuwa wanakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara hali inayopelekea wanachuo kushindwa kujisomea nyakati za usiku na barabara kushindwa kupitika kipindi cha mvua.

 "Kwa sasa chuo kimeanza kutoa fomu za Usajili kwa Muhula unaoanza Mwezi January 2023 kwa Fani za Umeme na Ushonaji na unaweza kuwasiliana nasi kupitia 0765907420 au website yetu https://shynetvtc.ac.tz/",amesema Abubakari.

“Mgeni Rasmi chuo chetu kwa sasa tunakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa umeme pamoja na ubovu wa miundo mbinu ya barabara ya kuja chuoni hivyo wanafunzi wengi kushindwa kujisomea nyakati za usiku na barabara kushindwa kupitika kipindi cha mvua”, amesema Abubakari.

Pia, amesema changamoto nyingine ambayo inawakabili chuoni hapo, ni ukosefu wa huduma ya maji ambapo huingia gharama ya kuchimba visima na kutumia sola na jenereta wakati wa kusukuma maji.

Katika hatua nyingine ametoa wito kwa wazazi, kuwasaidia watoto wao ambao wanahitimu mafunzo mbalimbali ya ufundi chuoni hapo kwa kuwanunulia vifaa au kuwapatia fedha za mitaji ili wajiajiri wenyewe, kuliko kuwaacha wakilandalanda mitaani na kulalamika hakuna ajira na wakati wana ujuzi wa kutosha.

Aidha Mwanafunzi Catheline Leonard akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wenzake, amesema changamoto kubwa ambayo inawakabili wahitimu wa mafunzo ya ufundi ni ukosefu wa ajira na fedha za mitaji ili wapate kujiajiri wenyewe na ndiyo maana wengi wao huishia mitaani na kukaa bila kazi.

Kwa upande wake Diwani wa kata ya Lubaga Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga Reuben Dotto , amewatoa wasiwasi wahitimu wa ShyNet  hasa wale ambao wanaishi Manispaa ya Shinyanga ,kuwa hakuna ugumu wowote wa kupata fursa zilizopo katika kata hiyo na Manispaa kwa ujumla kwa kuwa wana ujuzi unaweza kuwasaidia kujikwamua kimaisha.

Dotto ametoa ahadi pia kwa wahitimu wa fani ya umeme kuwa ataangalia namna ya kuwasaidia wale wanafunzi wa fani za umeme kwa kuwaombea kazi kwenye miradi mbalimbali ya manispaa hiyo ikiwamo ya ujenzi wa vituo vya afya, zahanati,Sekondari , huku akiwasihi wasione aibu kufungua ofisi yao na kujiajiri wenyewe hali itakayo wewezesha wahitimu kumudu soko la ushindani kwenye ajira, a

Akizungumzia suala la changamoto ya Umeme ,maji ,na barabara Dotto , amesema atafuatilia kuhakikisha changamoto hizo zinatatuliwa kwa haraka ikiwemo kuhamasisha jamii kupeleka watoto wao wanao hitimu elimu ya kidato channe katika shule hiyo ili kuongeza idadi ya vijana wenye ujuzi katika kata hiyo na manispaa kwa ujumla.
Mgeni Rasmi Reuben Dotto akizungumza na wazazi na walezi pamoja na wahitimu kwenye mahafali ya Kwanza ya Chuo cha ShyNet 
Mkuu wa chuo cha ShyNet Abubakar Rehani akitoa taarifa ya chuo hicho.

Wahitimu mwaka wa Pili Chuo cha ShyNet wakimwelezea mgeni rasmi mbinu mpya ya kuunganisha umeme majumbani.
Mgeni rasmi Leuben Dotto pamoja na Mkuu wa chuo cha ShyNet  Abubakar Rehani wakisikiliza maelezo kutoka kwa wahitimu
Mkuu wa chuo cha ShyNet  Abubakar Rehani pamoja na mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto wakiangalia Nguo zilizoshonwa na wahitimu wa fani ya Ushonaji .
Mhitimu Catheline Leonard akisoma risala kwa niaba ya wahitimu wengine.
Mkuu wa chuo cha ShyNet Abubakar Rehani akimuongoza mgeni rasmi Mhe. Reuben Dotto na kumuonesha mazingira ya chuo.
Wanachuo wa mwaka wa kwanza wakielezea ujuzi walio pata mpaka sasa katika fani ya umeme.
Wahitimu wa mahafali ya kwanza chuo cha ShyNet  wakiimba wimbo maalum
Wahitimu wakionesha mtindo wa mavazi.
Mhitimu akionesha mtindo wa mavazi.
Wahitimu wakionesha mtindo wa mavazi.
Mkuu wa chuo cha ShyNet  Abubakar Rehani akiwaonyesha mazingira ya chuo wageni waalikwa pamoja na wazazi .
Mkuu wa chuo cha ShyNet Abubakar Rehani akiwaonesha mazingira ya chuo wageni waalikwa pamoja na wazazi .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments