JAMAA AKAMATWA NA BASTOLA BANDIA AKIJIFANYA MWANAJESHI



Nguo za kijeshi

Jeshi la Polisi mkoa Tanga linawashikilia watu wawili akiwemo Rodrick Masawe mkazi wa wilaya ya Muheza kwa tuhuma za kukutwa na bastola (Pistol) bandia iliyotengenezwa kienyeji akiitumia kufanyia vitendo vya uhalifu huku akijifanya kuwa ni mtumishi wa serikali wa jeshi la JWTZ.


Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Henry Mwaibambe, amesema watuhumiwa hao wamekuwa wakitumia silaha hizo kwenye matukio mbalimbali ya kihalifu.

Kamanda Mwaibambe amesema Rodrick Masawe alikamatwa katika Kijiji cha Mamboleo wilayani Muheza akiwa na bastola hiyo bandia na kujifanya mtumishi wa serikali wa jeshi la JWTZ ambapo mtuhimiwa huyo yupo mbaroni kwa hatua za kisheria.

Aidha Kamanda Mwaibambe ameelezea mtuhumiwa mwingine Huruma John ambaye pia alikamatwa na bastola bandia alikutwa eneo la Kisosora, Kata ya Nguvumali, Tarafa ya Chumbageni jijini Tanga akiwa na silaha hiyo kwenye begi lake la mgongoni ambapo mtuhimiwa anaendelea kuhojiwa na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

CHANZO - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments