ATENGWA NA JAMII BAADA YA KUZAA WATOTO 11 WOTE VIPOFU


Mwanamke ameelezea kwa hisia kuhusu kutengwa na jamii na marafiki baada ya kuzaa watoto 11 na ambao wote ni vipofu.


Katika Makala ambayo yalipakiwa na blogu ya YouTube, mama huyo kwa jina Agnes Nespond alieleza kwamba baada ya muemwe kufariki kwa zaidi ya miaka 20 iliyopita, amekuwa akipitia ugumu kuwalewa watoto wake 11 ambao wote wana ulemavu wa macho.


Alisema kuwa watoto wote hao ambao wengine wameshakua watu wazima kanisa hawawezi kujitegemea kutokana na ulemavu wa macho amabo umewaweka chini ya uangalizi wake katika kumudu mahitaji yao yote kutoka kula, kunywa na mahitaji mengine ya msingi.


Alisema kwamba tatizo hilo lilikuwa likiwapata watoto wake mmoja baada ya mwingine na aliendelea kujitahidi kuzaa kwa tumaini kwamba angezaa mtoto angalau mmoja mwenye anaona lakini wote kumi na moja wakawa na tatizo lile lile.


Licha ya madaktari kumhakikishia kila mara kwamba watoto wake watakuwa wakamilifu, walikuwa vipofu kila wakati baada ya kuzaliwa. Alichukua jukumu la kuchimba mizizi ya historia yake ili kuangalia ikiwa ni suala la urithi.


Hata hivyo, Nespondi hakuweza kupata kiini chochote katika familia yake kuhusu upofu, isipokuwa wanafamilia wake ambao walikuwa na matatizo ya macho kutokana na umri wao.


Nespond ambaye ni mkaazi katika kijiji kimoja nchini Kenya ambacho wazalishaji wa Makala hawakuweka wazi alisema kwamba alianza kushuku huenda kuna mkono wa ushirikina katika tatizo hilo kwa wanawe ambao alisema licha ya kuwa watu wazima, bado wanamtegemea kutokana na kwamba hakuna mtu anayeweza kuwapa kazi.


“Kula ni shinda, kunywa ni shida sina mtu wa kunisaidia. Ni mimi tu peke yangu,” Nespond alieleza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments