TVLA YAKABIDHI MSAADA WA FIMBO 20 ZA WATU WENYE ULEMAVU TLB

Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akimkabidhi moja fimbo za watu wenye ulemavu Katibu wa Chama cha TLB, Bw.Protase Mutakyanga katika hafla ya utoaji msaada wa fimbo 20 kwa Chama hicho leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akimkabidhi boksi la fimbo za watu wenye ulemavu, Katibu wa Chama cha TLB, Bw.Protase Mutakyanga katika hafla ya utoaji msaada wa fimbo 20 kwa Chama hicho leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa fimbo 20 za watu wenye ulemavu kwa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa fimbo 20 za watu wenye ulemavu kwa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kukabidhi msaada wa fimbo 20 za watu wenye ulemavu kwa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam Katibu wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Bw.Protase Mutakyanga akizungumza mara baada ya kupokea msaada wa fimbo 20 za watu wenye ulemavu kutoka kwa Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA) leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam.Katibu wa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB), Bw.Protase Mutakyanga akitoa pongezi mara baada ya kupokea msaada wa fimbo 20 za watu wenye ulemavu kutoka kwa Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA) leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam


. *****************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

WAKALA ya Maabara ya Veterinari (TVLA) imekabidhi msaada wa fimbo 20 zenye thamani ya tsh. 1,000,000/= kwa watu wenyeulemavu wa macho (wasioona) kwa Chama cha Wasioona Tanzania (TLB) Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam ambazo zitawasaidia katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Oktoba 17,2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa makabidhiano hayo, Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Maabara ya Veterinari (TVLA), Dkt. Stella Bitanyi amesema kuwa wamekabidhi Fimbo hizo kama shukrani kwa mwenyezi Mungu kwa yale ambayo wametendewa na pia kuguswa na hali ambayo wanapitia walemavu hao.

"Tumerudi kwao kuonesha shukrani kwa Mwenyezi Mungu, kwasababu hali ambayo wanapitia hawakuitaka wao ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu ambayo inaweza kumtokea mtu yeyote ambaye anaona leo". Amesema Dkt. Bitanyi

Aidha Dkt. Bitanyi amesema TVLA wamekuwa wakishashirikiana na makundi mbalimbali ya walemavu ikiwa kama uwajibikaji kwa kuwasidia watu wenye mahitaji kwenye jamii mfano kikundi cha Magomeni wameshapatiwa msaada kuchangia kupatikana kwa viti mwendo ambavyo  Chama kili kilikuwa kinafanya kukusanya kwa ajili ya wanachama wake. 

Nae Katibu wa Chama cha TLB, Bw. Protase Mutakyanga ameipongeza TVLA kwa msaada ambao wamewapatia kwani fimbo hizo ni ghali kwa mwananchi mmoja mmoja kwa wasioona ambapo imekuwa ni changamoto kwa upande wao kuzipata.

Hata hivyo Bw.Mutakyanga amewaomba TVLA kuendelea kufanya tafiti na kuzalisha na chochote kitachopatikana waendelee kutoa kwa watu wenye mahitaji maalumu ili kupunguza changamoto wanazokabiliana nazo.

Aliongeza kuwa walipeleka ombi lao mnamo Mei 24, 2022 na Mtendaji Mkuu wa TVLA aliwajibu barua yao kwamba Wakala wapo tayari kuwasaidia takribani fimbo 20 kwa ajili  ya wanachama wa chama hicho.

"Chama cha Wasiiona Wilaya ya Temeke kina jumla ya wanachama 223 ambapo wote ni wenye ulemavu wa macho ambao wanahitaji fimbo, tunashukuru kwa msaada huu kwasababu umekuja katika wakati muhimu sana kwani ni siku ya kesho tu tutaanza safari ya kuelekea mkoani Manyara kwa ajili ya maadhimisho ya kimataifa ya Fimbo  nyeupe". Amesema

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments