MO GREEN INTERNATIONAL YAJIPANGA KUHAKIKISHA INAINUA VIPAJI VYA MASUMBWI NCHINI

Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Geen International Bw.Kessa Mwambeleko akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro.
Bondia Twaha Kiduku akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro. Bondia Dulla Mbabe akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro. Bondia Karim Mandonga akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro. Bondia Saidi Mbelwa akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 12,2022 Jijini Dar es Salaam kuelekea pambano la ngumi litakalopigwa Novemba 25,2022 mkoani Morogoro.

*********************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mo Geen International Sports Promotion imeandaa pambano la ndondi mkoani Morogoro ikiwashirikisha mabondia nyota wenye historiia mbalimbali ndani na nje ya nchi, pambano ambalo litapigwa Novemba 25,2022.

Akizungumza leo Oktoba 12,2022 na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Mo Geen International Bw.Kessa Mwambeleko amesema mabondia takribani sita wataweza kushiriki siku hiyo akiwemo Twaha Kiduku, Dulla Mbabe na kari Mandonga ambapo wote hao wamepewa muda wa kuelezea walivyojipanga na wote wapo tayari kwa pambano na kuwapa wananchi burudani.

"Bondia nyota Twaha Kiduku, ambaye ana historia kushinda mikanda mbalimbali, atapambana na Bondia Damian Bonell kutoka nchini Argentina ambaye pia ana historia ya kusisimua kwenye tasnia ya ngumi". Amesema

Amesema Pambano lingine katika siku hiyolitawahusisha mabondia Dulla Mbabe ambaye mashabiki wake walikuwa na kiu ya kumuona ulingoni kwa muda mrefu, akipambana na bondia Mkongo, Mbiya Kanku.

Aidha pambano lingine litamuhusisha bondia aliyejipatia umaarufu mkubwa katika siku za hivi karibuni, Karim Mandonga atakayepambana na Bondia Said Mbelwa.

Nae Bondia Twaha Kiduku amewataka wapenzi ngumi waweze kushiriki kushuhudia burudani nzuri kutoka kwake na kuwahakikishia mashabiki ushindi dhidi ya mpinzani wake Muargentina Damian Bonell.

Pamoja na hayo ameupongeza uongozi wa kampuni ya Mo Geen International Sports Promotion kwa kuandaa pambano hilo ili mabondia wengine waweze kuonesha vipaji vyao katika tasnia ya ngumi na kuweza kupeperusha bendera ya taifa.

Kwa upande wake Karim Mandonga amesema atahakikisha anashinda pambano hilo na kumtambia mpinzani wake kuwa atampiga na kutoa burudani kwa mashabiki wake ambao wamekuwa wakimshangilia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments