MAITI YAGOMA KUSAFIRISHWA KWA GARI LA KIFAHARI

Shughuli zilisimama katikati ya mji wa Kitale (CBD) nchini Kenya wakati gari la kubeba maiti lililokuwa limebeba mwili wa mfanyabiashara mashuhuri lilipokataa kusonga na kuwavutia wakazi waliofurika kushuhudia tukio hilo la ajabu.

Mmoja wa walioshuhudia tukio hilo alisema lilidumu kwa zaidi ya dakika thelathini na watu wengi walishangazwa kushuhudia tukio hilo lisilo la kawaida.

 "Tumeshtuka kwa sababu hatujawahi kupata matukio ya aina hii katika mji huu. Mara nyingi tunatazama matukio kama haya kwenye televisheni na kuyasikiliza kwenye redio,” shahidi huyo alisema.

Baadaye mwili huo ulitolewa kwenye gari hilo la kifahari aina ya Mercedes Benz na kuhamishiwa kwenye gari lingine la kubeba maiti aina ya Toyota Hilux na kisha msafara uliokuwa ukiongozwa na Bendi ya Jeshi la Wokovu ukaendelea.

Mmoja wa wanabiashara mjini humo Ken Mutai, alifutilia mbali tukio hilo kuwa la kushangaza akisema kuwa gari hilo la maiti lilikuwa na matatizo ya kiufundi.

"Sitaki kuamini kile ambacho watu wengine wanasema kwamba mwili ulikataa kupelekwa nyumbani. Tatizo la kiufundi linawezekana na kwa hivyo kilichotokea si cha ajabu kwangu,” Mutai alisema.

 Katika mahojiano na K24, Mzee wa jamii ya Bukusu ambaye jina aliomba jina lake kubanwa alisema tukio hilo lilitokana na tafsiri ya kitamaduni.

 “Huenda mwili ulikataa kurudishwa nyumbani kwa sababu mtu aliyehusika na kifo chake alikuwa eneo hilo, au kwamba baadhi ya matakwa yake yalikuwa hayajatimizwa, pengine marehemu hakutaka kubebwa kwenye gari la gharama au hakutaka kufika nyumbani mapema,” alisema mzee huyo.

Via Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments