SHAKA : RAIS SAMIA NI PUMZI MPYA KWA MAENDELEO YA NCHI

Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka, amesema kutokana na kasi ya kutekeleza miradi ya maendeleo nchini, Rais Samia Suluhu Hassan ni pumzi mpya kwa maendeleo ya nchi.


Shaka amesema hayo leo Oktoba 15, 2022 katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Rais Samia ukiwa ni sehemu ya ziara yake mkoani Geita, Shaka akitoa salamu za CCM alitumia fursa hiyo kueleza kuwa tangu Rais Samia alipoingia madarakani mambo makubwa yamefanyika.

"Sisi ambao tumekuwa na wewe leo tangu asubuhi ni mashahidi, tumekwenda pale katika Hospitali ya Kanda ya Chato. Hospitali ile ni ukombozi mkubwa kwa wananchi kwa kuwa itatibu hata magonjwa sugu," amesema.

Shaka amesema mbali na Hospitali ya Kanda ya Chato, katika eneo la Kanda ya Ziwa pia kuna hospitali nyingine kubwa ikiwemo ya Bugando ambayo inashiriknai na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kutoa matibabu ya saratani na Hospitali ya Nyerere iliyopo Musoma mkoani Mara ambayo inashirikiana na Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) kutibu matatizo ya mifupa.

Mbali na sekta ya afya, Shaka amesema Rais Samia ameendelea kutekeleza ahadi mbalimbali zilizotolewa kwa ajili ya kuleta maendeleo

"Sasa ni wakati wa kwenda bega kwa bega na Rais Samia kuleta maendeleo. Rais Samia ni pumzi mpya ya maendeleo kwa nchi yetu," amesema.

Shaka ametumia fursa hiyo kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Rais Samia katika kuleta maendeleo kwa kuwa tangu ameingia madarakani hakuna kilichosimama.

Aidha, ametahadharisha na kuonya kuhusu rushwa katika kusimamia miradi ya maendeleo na kusema Chama kitaendelea kuwa karibu katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo.
Maelfu ya Wananchi waliojitokeza mji wa Buseresere/katoro leo Oktoba 15,2022 mkoani Geita wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (hayupo pichani) Mhe.Samia Suluhu Hassan aliposimama na kuwasalimia wakati akielekea Geita mjini kukagua miradi ya maendeleo.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan leo Jumamosi tarehe 15 Oktoba, 2022 amekutana na kuzungumza na wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Geita.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments