BENKI YA KCB YAVUKA UZANIA WA TRILIONI MOJA

 

Mkurugenzi wa fedha -KCB Willis Mbatia (kulia) upande wa kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa -KCB Cosmas Kimario.


Mkurugenzi mtendaji wa -KCB Cosmas Kimario (katikati) upande wa kulia ni Mkurugenzi wa fedha -KCB, Willis Mbatia pamoja na mwenyekiti wa bodi KCB John Ulanga.

Menejimenti ya bank ya -KCB ikiongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa -KCB Cosmas Kimario (wapili kutoka kulia walioketi)

........................
NA ISSA MOHAMED

Benki ya –KCB imefikia kiwango cha uzania wa mali ya zaidi shilingi trilioni moja sawa na ukuaji wa zaidi ya asilimia 100 katika kipindi cha robo tatu ya mwaka huu hatua iliyotajwa kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa wateja na kutekeleza mipango ya kukuza biashara.

 

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na Mkurugenzi mtendaji wa –KCB, Cosmas Kimario ambapo amesema rekodi hiyo imechangiwa na ongezeko la amana za wateja kwa asilimia 105 katika kipindi cha miaka mitano.

 

Amesema faida ya benki hiyo imeongezeka kwa asilimia zaidi ya 100 hadi kufikia shilingi bilioni 22.4 huku sababu nyingine ni kuwajali wateja wa benki hiyo ikiwemo kuwainua wafanyabiashara wadogo na wakati -SME's hasa kujikita katika huduma za kidigitali.

 

‘’Hali ya uchumi imekuwa nzuri kutokana na sera nzuri ya serikali ya awamu ya sita pamoja na benki kuu katika kusupport mabenki nchini hili limechangia katika kusaidia biashara za wateja wetu kukua’’ Amesema Cosmas

 

 

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya –KCB, John Ulanga amesema tayari benki hiyo imetenga zaidi ya bilioni 2. ili kuisaidia jamii hasa vijana ili kujiajiri kupitia program ya –KCB 2jiajiri.

 

‘’Sisi kama board mikakati yetu ni kuendekea kukua pamoja na kupanua biashara zetu hasa kwa upande wa faida, matumizi ya teknolojia pia imechangia kuwafikia wateja wengi zaidi’’ Amebainisha bwana John.

 

Naye mkurugenzi wa fedha –KCB, Willis Mbatia amesema utoaji wa mikopo umeongezeka kutoka bilioni 330 mwaka 2017 hadi bilioni 623 mwaka 2022 sawa na ongezeko la asilimia 88.

 

Itakumbukwa kuwa  benki kuu Nchini –BOT  ilizielekeza taasisi za kifedha nchini kupunguza mikopo chechefu ambapo –KCB imelitekeleza hilo kwa kushusha hadi asilimia 3 kutoka asilimia 17.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments