GGML WATUMIA BILIONI 1 KUSIMIKA MTAMBO WA PEKEE AFRIKA MASHARIKI, KATI WA KUCHENJUA KABONI (MAKINIKIA)

Meneja wa Idara ya Uchenjuaji, Elibariki Andrew (wa pili kutoka kushoto) akitoa maelezo kwa Waziri wa Madini, Dk. Doto Biteko aliyetembelea mgodi huo na kushuhudia mtambo wa uchenjuaji kaboni ulionunuliwa na kusimikwa kwa thamani ya Sh bilioni moja. Kushoto ni Mkurugenzi wa GGML, Terry Strong na Makamu Rais wa AngloGold anayeshughulikia Miradi Endelevu Ghana na Tanzania, Simon Shayo.
Mtambo wa uchenjuaji kaboni maarufu kama makinikia ulionunuliwa na kusimikwa mkoani Geita kwa thamani ya Sh bilioni moja na Kampuni ya GGML. Mtambo huo wa kwanza Tanzania, Afrika mashariki na kati utawezesha serikali kuongeza mapato pamoja na ajira katika sekta ya madini.
 ***

KATIKA kutekeleza mpango wa kulinda mazingirapamoja na kuunga mkono juhudi za Serikali kuifanyaTanzania kuwa nchi ya viwanda ifikapo 2025, Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imenunua nakusimika mtambo wenye thamani ya Sh bilioni moja kwa ajili ya kuchenjua kaboni ‘makinikia’ yanayotokanana shughuli za uchimbaji wa madini ya dhahabu.


Hatua hiyo inaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza napekee katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwana mtambo huo kwani hapo awali kampuni hiyo ilikuwainafuata huduma hiyo Afrika Kusini.


Hayo yamebainishwa hivi karibuni katika ziara yaWaziri wa Madini, Dotto Biteko ambaye alitembeleakampuni hiyo mkoani Geita kwa lengo la kujuamaendeleo ya GGML baada ya kuanza shughuli zauchimbaji wa chini ya ardhi katika migodi yake mitatu.


Akimkaribisha waziri huyo, Makamu Rais waAngloGold Ashanti anayeshughulikia Miradi endelevu kwa upande wa Ghana na Tanzania, Simon Shayo alisema mradi huo utaongeza mapato kwa serikali nakampuni hiyo kwa ujumla.


“Mradi huu wa kuchenjua mabaki ya kaboniunatusaidia kuhakikisha hatuyatupi mabaki yadhahabu na mabaki yenye asili ya hewa ukaayanayoingia kwenye mazingira … kwa sababu dunianzima ipo kwenye mapambano ya kupunguza hewa ukaa,” alisema.


Aidha, akizungumzia mradi huo, Dk. Biteko alisemaawali kaboni zilizokuwa zinazalishwa kwenye migodiiliyopo nchini zilikuwa zinasafirishwa kwenda nje ya nchi.

“Tulizuia watu wakadhani tunafanya kitu kibaya, sasa GGML wameweka mtambo mpya ambao umegharimu sh bilioni moja kwa ajili kuprocess upya kaboni zadhahabu na kupata dhahabu safi badala ya kusafirishaile kaboni kupeleka nje ya nchi,” alisema.


Alisema mbali na manufaa ya mapato ambayo nchiinapata, pia watu wengi wameajiriwa kwenye mtambohuo na kuondokana na umaskini.

“Lakini pili teknolojia ya kaboni hizi ambazozinazalishwa kwenye migodi mingine zitakuwazinafanyiwa processing hapa nchini hasa ikizingatiwaile kaboni ina dhahabu.

“Mahali pengine unaweza kuona ile kaboni imetupwakama uchafu, lakini kwa taarifa tuliyopewa itazalishazaidi ya gramu 80,000, ni dhahabu nyingi zaidi ya kilo 80 kwa kaboni hii na bado itaendelea kuzalishwa maranyingi. Kwa hiyo tutapata mapato mengi zaidi,” alisema na kuongeza;

“Hakuna mgodi mwingine ambao umetengenezamtambo wa kuchenjua hiyo kaboni Afrika mashariki nakati kwa hiyo teknolojia hii sisi tumekuwa walimu, nawapongeza GGML kwa ubunifu huo,” alisema.


Naye Mbunge wa Geita Mjini, Constantine Kanyasu(CCM) aliipongeza kampuni hiyo kwa hatuailizochukua kuhakikisha kuwa inapanua wigo waupatikanaji wa ajira kwa Watanzania.


“Mathalani tukizungumzia local content tulitaka iwelocal of the local, nauona ushawishi huo unafanikiwa kwa sababu sasa katika maeneo mengi ambayo nimekwenda nimeona ushiriki wa watu wa Geita kwenye shughuli mbalimbali za uchumi wa mgodi,” alisema.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments