WAVAMIZI HIFADHI YA MSITU WA BONDO WATAKIWA KUONDOKA


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akijibu maswali Bungeni jijini Dodoma leo Septemba 19,2022.

…………………………

Wananchi waliovamia Hifadhi ya Msitu wa Bondo wametakiwa kuondoka ndani ya hifadhi hiyo ifikapo Desemba 30,2022.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Kilindi Mhe. Omar Mohamed Kigua bungeni jijini Dodoma leo Septemba 19,2022.

“Kwa nyakati tofauti hifadhi hii imekuwa ikivamiwa kwa ajili ya shughuli za kibinadamu zikiwemo kilimo,makazi na kuchungia mifugo” Mhe. Masanja amefafanua.

Amesema Serikali imeweka matangazo ya kuwataka wananchi wote kuondoka ndani ya hifadhi hiyo.

Aidha, amesema Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya inaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali misitu nchini.

Hifadhi ya Msitu wa Bondo, ipo katika Kijiji cha Mswaki,Kata ya Msanja Wilayani Kilindi Mkoani Tanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments