WASINDIKAJI WA VYAKULA WATAKIWA KUWEKA WAZI USINDIKAJI



Na Imma Msumba ; Arusha

Wasindikaji wa vyakula pamoja na Wafanyabiashara wametakiwa kuwa na utaratibu unaoonesha mchanganyiko unaotumika katika bidhaa zao ili kumruhusu mlaji kufanya maamuzi kabla yakufanya manunuzi nakujiepusha na magonjwa yasiyo ambukiza yanayotokana na baadhi ya vyakula.

Mtaalamu wa Afya na Mazoezi kutoka shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyo ambukiza, Dkt. Waziri Ndonde akizungumza jijiji Arusha wakati wa majadiliako yakufikisha elimu kwa jamii namna yakujiepusha na tabia bwete na ulaji wa vyakula usiozingatia viwango, ambaye amesema watu wengi hununua vyakula bila kuzingatia mchanganyiko uliopo nakupata athari.


Dkt. Ndonde amesema kuwa kwa sasa Wanafanya tafiti zitakazosaidia kuondokana na kasi ya kuenea kwa magonjwa yasiyo ambuliza yanayo sababishwa na matumizi ya vyakula visivyo faa.


Pia Dkt Ndonde, ameongeza kuwa namna pekee itakayo saidia kuepukana na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo kisukari pamoja na magonjwa ya moyo ni pamoja na kuacha tabia bwete na kuanza kufanya mazoezi ikiwa ni njia pekee ya kupunguza athari zitokanazo na matumizi ya vyakula.


Hata hivyo Dkt Ndonde amesema ipo haja ya mamlaka zinazo simamia chakula na dawa kutunga sheria madhubiti pamoja na kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya vyakula na dawa ikiwa ni mpango wa kusaidia Afya ya jamii.











Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments