TCRA: JAMII YOTE ISHIRIKI KUWALINDA WATOTO DHIDI YA UKATILI MTANDAONI


************************

li kuwalinda Watoto dhidi ya ukatili mtandaoni jamii nzima inapaswa kuhusika wakiwemo Watunga Sera, Asasi za Kiraia, Viongozi wa Dini, Mamlaka za Usimamizi wa Sheria na jamii yote. Aidha imebainishwa kuwa ukatili wa Watoto mtandaoni unaweza kukoma ikiwa jamii yote itashirikiana kutokomeza matukio ya ukatili.

Akizungumza katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na kituo cha redio One jijini Dar es salaam Afisa Mawasiliano Mwandamizi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Semu Mwakyanjala alibainisha kuwa pamoja na Sheria zinazowalinda Watoto dhidi ya unyanyasaji na udhalilishaji kuwepo ikiwemo sheria ya makosa mtandaoni ya 2015, bado jamii inapaswa kushiriki kikamilifu kuwalinda Watoto dhidi ya ukatili kwenye mtandao.

“Mambo ya kihalisia katika ulimwengu wetu hayapo tofauti na yale yanayotendeka kwenye mifumo ya mtandao, hivyo ikiwa tunawalinda Watoto dhidi ya ukatili kwenye ulimwengu wa kawaida, vivyohivyo tuwajibike kuwalinda katika mazingira ya kimtandao na kwenye mifumo yote ya mawasiliano,” alisisitiza Mwakyanjala.

Afisa huyo aidha, alisisitiza umuhimu wa waandaaji wa maudhui mtandaoni pamoja na waundaji wa mifumo ya Mawasiliano inayobeba maudhui kuhakikisha wanaweka miundombinu inayowalinda Watoto wakati wanapolazimika kuingia kwenye mitandao kwa shabaha ya kujifunza na kupata elimu.

“Waandaaji maudhui wanatakiwa wahakikishe maudhui wanayotengeneza yanakuwa yenye staha, yasiwe yenye kuhamasisha ukatili dhidi ya watoto,” alisisitiza

Shirika la Umoja wa Mataifa la Watoto (UNICEF) linabainisha kuwa ukatili dhidi ya Watoto umekuwa ukiongezeka hasa miongoni mwa Watoto wa kike ambapo Sheria ya Makosa ya Mtandao ya 2015 kifungu cha 13 inatoa katazo la kuchapisha ponografia za Watoto kwenye mifumo ya kompyuta, aina ya ukatili ambapo UNICEF inaeleza umekuwa ukiongezeka kwa kasi kwenye mazingira ya mtandao

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments