SEKTA BINAFSI ZAKARIBISHWA KUWEKEZA KWENYE KILIMO CHA MAUA MKOANI NJOMBE

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24,2022 kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani Njombe.  Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24,2022 kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani NjombeKaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Bw.Felix John akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24,2022 kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani Njombe

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imepanga kuzindua mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini kwani kumekuwa na vivutio vingi ikiwemo hifadhi ya Taifa ya Kitulo ambayo nimaalufu duniani kwa maua.

Jambo hilo linatarajia kufanyika Septemba 26,2022 ambapo wataanza Septemba 25 kwa maonesho katika ukumbi wa Njombe Mji na siku ya tarehe 26 watayahitimisha kwa uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa utalii.

Ameyasema hayo leo Septemba 23,2022 Jijini Dar es Salaam,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Bw.Felix John wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea uzinduzi wa mkakati wa utangazaji wa Utalii katika mikoa ya Kusini ambao utafanyika Septemba 26,2022 mkoani Njombe

Amesema mkakati huo ni sehemu ya utekelezaji wa malengo mahususi ya Tanzania the Royal Tour ambalo lakwanza lilikuwa ni kutangaza vivutio vyakipekee vya utalii wa nchi yetu na kuvutia wawekezaji kuwekeza katika sekta mbalimbali za uchumi wa nchi yetu.

"Njombe kuna fursa kama ilivyo maeneo mengine ya nchi na ndo maana tumeamua sasa kuffanya huu uzinduzi kule Njombe na sio Kusini mwa Tanzania kama ilivyozoeleka". Amesema Bw.Felix.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Anthony Mtaka amesema mkoa huo utafanya kazi kwa ukaribu na TTB na kuwaomba waweze kuwaambiia wananchi kuwa Njombe inazo fursa nyingi kwenye eneo la utalii kama vile hiffadhi ya kitulo ambayo ni maarufu na maalumu kwa maua ambayo hayapatikana kwa wingi katika ameneo mengine duniani.

Aidha amewakaribisha watanzania ambao watatakiwa kuwekeza katika sekta ya Utalii kwenye mkoa huo kwenye mahoteli au kuwekeza kenye kilimo cha maua ya kibiashara.

"Niwakaribisha sekta binafsi ambao watahitaji kufanya kilimo cha maua kama ambavyo kilimo hiki cha maua yakibiashara inafanyika Moshi na Arusha, niwakaribishe Njombe fursa hiyo ipo". Amesema Mhe.Mtaka

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments