NIC KUSAIDIA MASUALA YA BIMA KWA SERENGETI GIRLS KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 40 kwaajili ya kuiunga mkono timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na timu ya taifa ya Walemavu (Tembo Warriors National Team) wakati wakijiandaa kwenda kushiriki kombe la dunia.Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akimkabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni 40 kwaajili ya kuiunga mkono timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) katika hafla ya kuwaaga wachezaji hao ambao wanakwenda kushiriki kombe la Dunia.Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 40 kwaajili ya kuiunga mkono timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) pamoja na timu ya taifa ya Walemavu (Tembo Warriors National Team) katika hafla ya kuwaaga wachezaji hao ambao wanakwenda kushiriki kombe la Dunia.Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam.Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akimkabidhi bendera kwa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) katika hafla ya kuwaaga wachezaji hao ambao wanakwenda kushiriki kombe la Dunia.Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akipokea vifaa vya michezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Bw.Felix John kwaajili ya timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) katika hafla ya kuwaaga wachezaji hao ambao wanakwenda kushiriki kombe la Dunia.Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akimkabidhi vifaa vya michezo nahodha wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) katika hafla ya kuwaaga wachezaji hao ambao wanakwenda kushiriki kombe la Dunia.Hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akizungumza katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa akisisitiza jambo wakati akizungumza katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Hassan Abbasi akizungumza katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye akizungumza katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam.Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw.Wallace Kalia akizungumza katika hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi wa Michezo nchini Bw.Ally Mayayi Tembele akifuatilia hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Baadhi ya viongozi wa mpira wa miguu nchini wakifuatilia hafla ya kuwaaga wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam. Wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) wakiwa kwenye hafla ya kuagwa kwenda kushiriki kombe la Dunia. Wachezaji hao wameagwa leo na kukabidhiwa bendera, bima na vifaa vya michezo ambapo hafla hiyo imefanyika leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SHIRIKA la bima la Taifa (NIC) limekabidhi shilingi Milioni 40 kwaajili ya kuiunga mkono timu ya taifa ya mpira wa miguu ya wasichana U-17 (Serengeti Girls) pamoja na timu ya taifa ya Walemavu (Tembo Warriors National Team) pamoja kutoa bima zitakazowalinda wakipata majanga wakati wakiwa nje ya nchi.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga Serengeti Girls leo Septemba 21,2022 Jijini Dar es Salaam, Waziri wa Utamduni, Sanaa na Michezo Mhe.Mohamed Mchengerwa ameipongeza NIC kwa kuamua kushiriki kwa namna moja katika kusaidia timu hiyo kwenda kufanya vizuri katika michuano ya kombe la Dunia.

Aidha amewataka wachezaji wakapambane na kuweza kufanya vizui kwenye michuano hiyo kwani uwepo wa bima hiyo itaweza kuwasaidia pindi wanapopata changamoto katika michezo waweze kusaidika kwa urahisi na kwa haraka.

Hata hivyo amewataka wachezaji hao kuwa wazalendo wa nchi yao kwa kuhakikisha wanapambana na kufanikiwa kufanya vizuri kwenye michuano hiyo ambayo inatarajia kufanyika hivi karibuni.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elirehema Doriye amesema kuwa kwa wale wachezaji watakaoumia kila wiki watakuwa wanapewa laki moja kwa kipindi ambacho amekaa mpaka kufikia milioni 10, hivyo amewataka wachezaji hao kupambana na wasiogope kuumia.

Amesema timu hiyo ikifanya vizuri na kufika hatua ya robo fainali, watazawadiwa kiasi cha shilingi milioni 40, wakifika nusu fainali watawazawadia shilingi milioni 80 na wakifika hatua ya fainali watapatiwa milioni 100.

"Mnatakiwa mkapambana na kuhakikisha mnaipeperusha vizuri bendera ya Tanzania, mkafanye vizuri na msigope kuumia hata hivyo ikitokea imchezaji akapata kilema cha kudumu atalipwa hivyo basi NIC ipo kwaajili yenu na tunawatakia kila la heri kwenye michuano hiyo". Amesema Bw.Doriye

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments