PROF. MKENDA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA SINGAPORE NCHINI DOUGLAS FOO



Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Septemba 2,2022 jijini Dar es Salaam amekutana na kufanya mazungumzo na balozi wa Singapore nchini Bw.Douglas Foo.


Katika mazungumzo hayo Tanzania na Singapore zimekubaliana kuboresha ushirikiano zaidi katika sekta ya elimu ikiwemo kubadilishana uzoefu kwa walimu na wakufunzi kutoka taasisi za elimu za nchi hizo.


Akizungumza katika kikao hicho Prof. Mkenda amesema mfumo wa elimu nchini Singapore umewezesha kupambana na tatizo la ajira katika nchini humo, hivyo Tanzania itapata uzoefu huo kupitia timu zinazohusika na uboreshaji Sera na mabadiliko ya mitaala.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments