JAFO AFANYA ZIARA KATIKA MACHIMBO YA VIFUSI MBUTU KIGAMBONI


************************

Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe Dkt. Selemani Jafo amefanya ziara ya ukaguzi wa Mazingira katika machimbo ya Vifusi vya kokoto yaliyopo Mbutu Kigamboni jijini Dar es salaam mapema leo tarehe 30 septemba 2022.

Waziri Jafo mara baada ya kufika katika eneo la Mbutu Kigamboni hakufurahishwa na namna shughuli za uchimbaji zinavyofanyika katika eneo hilo kwani hazizingatii utunzaji na uhifadhi wa Mazingira na mmiliki wa machimbo hayo hajafanya Tathimini ya Athari Kwa Mazingira na Wala hana cheti Cha Mazingira kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.

Aidha waziri Jafo amemtaka mmiliki wa machimbo hayo kufanya Tathimini ya Athari Kwa Mazingira na kufika katika Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC kujisajili na kupata cheti Cha Mazingira ili kuweza kuepusha madhara yanayoweza kutokea katika machimbo hayo na watu wengi waendesha familia zao Kwa kuchimba kokoto hizo.

"Wawekezaji wote kama mmewapa eneo hili Kwa ajili ya uchimbaji wa kifusi lazima wawe na cheti Cha kibali cha Mazingira kisajiliwe katika ofisi za NEMC na cheti kiainishe aina ya kazi itakayofanyika katika eneo hili". Amesema

Na Kwa upande wake meneja wa NEMC Kanda ya Mashariki Kusini Bw. Hamad Taimuru Kissiwa amewataka wamiliki wa machimbo hayo kufika katika ofisi za Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC ili kusajili machimbo hayo na kufanya Tathmini ya Athari Kwa Mazingira ili kulinda Mazingira na viumbe hai wengine

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments