RAIS SAMIA : VIJANA WANAHANGAIKA NA SUPU YA PWEZA, VUMBI LA KONGO


Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema matatizo mengi yanayowakumba vijana nchini kwa sasa kiafya yanatokana na lishe duni huku matatizo hayo yakiendelea kuwa siri hivyo kuagiza kufanyika utafiti wa kwanini vijana balehe wanamatizo ya lishe ili kuepuka kuwa na Taifa goigoi.


Rais Samia ameyasema hayo leo Ijumaa Septemba 30, 2022 wakati wa hafla ya utiaji saini mkataba wa usimamiaji shughuli za lishe jijini Dodoma.


Amesema wakati wakutafuta watoto vijana hao wanahangaika mara kunywa supu ya pweza na kwamba kuna tatizo ambalo wanalijua lakini wanalificha.


"Kwanini watoto wetu wakifika wakati wa kuongeza jamii wanahangaika, mara supu ya pweza,mara udongo wa kongo (Vumbi la Kongo) tuna tatizo na mnalijua mnalificha watafiti fanyeni utafiti, na kwa sababu halisemwi ni siri linaumiza zaidi vijana wetu, tatizo kubwa lipo kwenye lishe. Sasa watafiti fanyeni tafiti vijana wetu waweze kuzaa watoto wenye afya,”amesema.


Aidha amesema kama hali hiyo haitatafutiwa suluhu basi hali itaendelea kuwa mbaya zaidi

"Tukiacha hali ikienda hivyo tunaenda kuwa na taifa goigoi, tunaenda kuwa na taifa lenye watu lakini sio rasilimali watu, ni watu ambao ni mzigo kwa taifa, na sio watu ambao watazalisha kwa ajili ya taifa",amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم