DITOPILE AMPONGEZA RAIS SAMIA KWA KUANDIKA HISTORIA KUFIKISHA UMEME WA GRIDI MKOA WA KIGOMA

 

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) Mkoa wa Dodoma, Mariam Ditopile, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuandika historia ya kufikisha umeme wa gridi mkoani kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania.


Akizungumzia mafanikio hayo katika sekta ya nishati nchini, Mariam ambaye ni Mjumbe Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini amesema kutokana na hatua hiyo serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) inakwenda kuokoa mabilioni ya fedha kwa kuzima majenereta yaliyokuwa yakitumia fedha nyingi kuzalisha umeme katika maeneo ambayo yamefikiwa na umeme wa gridi. 


"Umeme wa Grid ya Taifa kufika Kigoma ina maana Shirika la Tanesco linaenda kuokoa kiasi cha sh. bilioni 22. 4 kwa mwaka. Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetengeneza historia ya kipekee kwenye sekta ya nishati.

"Nampongeza sana Rais Samia na Serikali ya Awamu ya Sita ameandika historia, umeme wa Grid ya Taifa umefika Kigoma na kwa mara ya kwanza umeme umefika Kakonko na Kibondo haikuwa Rahisi," amesema.


Mariam amesema jana TANESCO imefanikiwa kuzima majenereta ya Kibondo, Ngara na Biharamulo na kuanza rasmi kutumia umeme wa Grid ya Taifa jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi ilipopata uhuru mwaka 1961, “Jambo hili limepigiwa kelele sana na sisi wabunge na sasa serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imetekeleza kwa vitendo."


Amesema Wizara ya Nishati chini ya Waziri wake January Makamba na watendaji wengine wamedhihirisha uongozi sio maneno bali ni vitendo kwa kuhakikisha Kigoma inaunganishwa na Grid ya Taifa “nawapongeza sana kwa kutekeleza maono ya Rais Samia na kutekeleza vyema Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020-2025."

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments