ABBASI :TANZANIA MWENYEJI MKUTANO WA MUSIC IN AFRICA


*************************

Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi leo Septemba 15, 2022 amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Taasisi ya Music in Africa ambao kwa kushirikiana na Wizara pamoja na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wanaandaa Mkutano mkubwa wa sekta ya muziki Afrika (Music in Africa Conference). 

 Kikao hicho kimefanyika katika ofisi za Bodi ya Filamu zilizopo Barabara ya Kivukoni, Utumishi jijini Dar es salaam, ambapo Dkt. Abbasi amesema, Tanzania imeteuliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo utakaofanyika Novemba 24-26, 2022. 

"Mkutano huo unatarajiwa kuleta fursa mbalimbali za kukutana na wadau mbalimbali wa muziki kutoka Afrika na duniani kwa ujumla ambapo wasanii mbalimbali watapata nafasi ya kutumbuiza" amesema Dkt. Abbasi.

 Amewataka Wasanii na wadau wa muziki nchini kuthibitisha ushiriki wao kupitia mtandao wa @musicinafricaofficial
Kikao na mwakilishi wa Music in Africa Eddie Hatitye kilihudhuriwa pia na mwakilishi wa Shirikisho la Muziki nchini Fareed Kubanda “Fid Q” na mwakilishi wa vyama vya muziki kutoka Chama cha Muziki wa Kizazi Kipya nchini (TUMA), Mike T.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments