DC MBONEKO AHAMASISHA WANANCHI KUENDELEA KUPATA CHANJO YA UVIKO - 19



Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye kikao cha kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MKUU wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, amewahamasisha wananchi kuendelea kujitokeza kupata chanjo ya UVIKO-19, ili kuimarisha kinga za miili yao, na kuepuka kupata madhara makubwa pale watakapoambukizwa virusi vya Corona.

Mboneko amebainisha hayo leo Septemba 7, 2022 wakati akifungua kikao cha uhamasishaji wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 katika Kata Nne za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, ambazo ni Lyamidati, Mwenge, Imesela, na Mwamala.

Amesema baada ya watu kupata chanjo ya UVIKO-19 maambukizi ya virusi vya Corona yamepungua hapa nchini, ambapo mtu akipata chanjo hawawezi kudhurika zaidi tofauti na wale ambao hawakupata chanjo hususani pale watakapopata maambukizi.

“Tunamshukuru Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutuletea chanjo za UVIKO-19 na kujali afya za wananchi wake, na wananchi wakiwa na afya njema watafanya vizuri shughuli za maendeleo,”amesema Mboneko.

“Wakati wa utoaji chanjo ya UVIKO-19 anzeni pia na Makundi maalum, wakiwemo wazee, wenye magonjwa sugu na watumishi, na pale penye changamoto nipeni taarifa ili tuitatue na zoezi hili lifanikiwa kwa asilimia 100 kwa kuchanja wananchi wengi,”ameongeza.

Katika hatua nyingine Mboneko ameonya upotoshaji juu ya chanjo ya UVIKO-19  na kubainisha kuwa chanjo ni salama na zinatolewa bure, na kuwataka wataalam watoe elimu ya kutosha kwa wananchi ili zoezi hilo lifanikiwe kama ilivyofanyika kwenye chanjo ya Polio.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge, amesema wamefanya kikao hicho cha kampeni ya kuhamasisha chanjo ya UVIKO-19 kwa kushirikiana na Shirika la USA PeaceCorps kwa kuanza na Kata Nne wilayani humo.

Amesema katika Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga lengo lao lilikuwa ni kuchanja watu chanjo ya UVIKO-19, 218,929 lakini watu waliopata chanjo kamili wilayani humo ni 120,107 na waliopata dozi moja ni 47,359.

Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Dk. Nuru Yunge akizungumza kwenye kikao cha kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa ya chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa ya chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Kikao cha hamasa chanjo ya UVIKO-19 kikiendelea.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akipiga picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufungua kikao cha hamasa ya chanjo ya UVIKO-19 Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

Picha za pamoja zikiendelea kupigwa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments