MLINDOKO ACHAGULIWA MWENYEKITI WA WAZAZI SHINYANGA MJINI..."SITAPENDA KUSIKIA UONGO UONGO"


Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi CCM wilaya Fue Mlindoko akitangaza matokeo ya wagombea.


Na Suzy Luhende , Shinyanga blog


Mwenyekiti wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini Fue Mlindoko amesema katika uongozi wake hatapenda kuona watu wachonganishi ,waongo wanaorudisha nyuma maendeleo ya jumuia hiyo,endapo wakionekana watu wa namna hiyo atapambana nao kwa kufuata sheria na kanuni na watatolewa mara moja ndani ya jumuia hiyo.

Hayo ameyasema jana kwenye kikao cha baraza la jumuia ya wazazi lililofanyika katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga la kuwachagua viongozi ambao walikuwa hawajachaguliwa, ambao ni katibu elimu malezi na mazingira na wajumbe wa kamati ya utekelezaji.


Mlindoko alisema hatapenda kusikia mambo ya uongo uongo katika jumuia yake, atawapenda watu wenye kutoa ushauri mzuri wa kujenga chama na kuleta maendeleo ndani ya chama na jumuia ya wazazi.


"Nawaombeni sana viongozi wenzangu uchaguzi umeisha tufanye kazi kwa pamoja tushirikiane, ili jumuia yetu iweze kusonga mbele, pia tutunze siri zetu za ndani za kimaendeleo na tufanye mabadiliko, ni vizuri tuweke alama nzuri katika jumuia yetu na kuitendea haki," amesema Mlindoko.


" Inatakiwa tuwe wazazi kweli tusimame katika eneo letu, kwa sababu sisi ndio wazazi walezi, tabia yangu ni kuleta mshikamano, tuwe na upendo wa hali ya juu tupendane zaidi na dhumuni letu ni kujenga timu yetu imara", aliongeza.


Kwa upande wake katibu wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga Doris Kibabi amewaomba viongozi wote waliochaguliwa wawe viongozi wa mfano waonyeshe alama kuwa wamefanya maendeleo furani wasiache madoa ambayo yatakuwa hayana faida kwa kizazi kijacho, pia aliwaomba wakemee masuala ya ukatili wanayofanyiwa watoto.

"Nina imani na viongozi mlionichagulia tutaanza kwa mchaka mchaka, pia viongozi wa kata nawaombeni muwe mnafanya vikao ndani ya miezi mitatu, kwani sisi wenyewe ndiyo tunaitengeneza jumuia yetu, mnatakiwa muonyeshe alama tusiache madoa ambayo yatakuwa hayana faida kwa kizazi chetu tufanye kitu chenye faida kwa kizazi chetu,pia tukemee matukio mbalimbali ya ukatili kwa watoto wetu na tusimamie masuala ya elimu ili watoto wetu watimize ndoto zao", alisema Kibabi.


Aidha katika uchaguzi huo Richard Chacha Mseti alichaguliwa kuwa katibu elimu malezi na mazingira ambaye alishinda kwa kura 51, ambapo wapiga kura walikuwa 56, pia walichaguliwa wajumbe wa kamati ya utekelezaji, ambao ni Zulfa Dali, Daniel Kapaya, Josephate Msozi, na Giti Mliga Boniface, ikiwa msimamizi wa uchaguzi huo alikuwa Kudely Sokoine ambaye alikuwa katibu elimu malezi na mazingira hakugombea tena nafasi.
Wajumbe wa jumuia ya wazazi wakitumbukiza kura zao kwenye sanduku la kupigia kura.
Wajumbe wa jumuia ya wazazi wakidumbukiza kura zao kwenye sanduku la kupigia kura
Aliyekuwa katibu elimu malezi na mazingira Kudely Sokoine akihesabu kura kwa uwazi kwenye baraza la wazazi wilaya shinyanga.
Katibu elimu malezi na mazingira Richard Chacha Mseti akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua.
Katibu elimu malezi na mazingira Richard Chacha Mseti akiwashukuru wajumbe baada ya kumchagua.
Wajumbe wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini wakisikiliza maelekezo.
wajumbe wa jumuia ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini wakipiga kura.
Wenyekiti wa jumuiya ya wazazi Fue Mlindoko akitangaza matokeo.
Doris Kibabi,Katibu wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Shinyanga mjini

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments