MAMIA WAJITOKEZA KUMZIKA RAJAB MASANCHE MJINI SHINYANGA

Mwili wa Marehemu Rajabu Masanche ukiwa umebebwa kwenda kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele katika Makaburi ya Waislamu Nguzonane Manispaa ya Shinyanga
Marehemu Rajabu Masanche enzi za uhai wake, akiendesha Baraza la Madiwani Manispaa ya Shinyanga akikaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo na saa chache baada ya kumaliza kuendesha kikao akafariki dunia. Soma pia :RAJAB MASANCHE AFARIKI DUNIA

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

Wakazi wa Manispaa ya Shinyanga, watumishi na viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwamo na Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu, wamejitokeza kwa wingi kushiriki mazishi ya Mkuu wa Idara ya kilimo, mifugo na uvuvi Manispaa ya Shinyanga Rajab Masanche.

Mazishi ya Rajab Masanche yamefanyika leo Septemba 29,2022 katika Makaburi ya Waislam Nguzonane Manispaa ya Shinyanga, ambapo alifikwa na umauti Septemba 28 mwaka huu majira ya alfajiri katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na amefariki akiwa na miaka 56.

Aidha, kabla ya kifo chake Septemba 27,2022 aliendesha Baraza la Madiwani akikaimu nafasi ya Mkurugenzi wa Manispaa hiyo.

Mwili wa Marehemu Rajabu Masanche ukiwa umebebwa kwenda kupumzishwa kwenye makazi yake ya milele katika Makaburi ya Waislamu Nguzonane Manispaa ya Shinyanga.

Mwili wa Marehemu Rajabu Masanche ukiingizwa Msikitini kwa ajili ya kuombewa dua na kisha kwenda kuzikwa katika Makaburi ya Waislamu Nguzonane Manispaa ya Shinyanga.
Mwili wa Marehemu Rahabu Masanche ukiwasili katika Makaburi ya Waislamu Nguzonane Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya mazishi.
Mwili wa Marehemu Rahabu Masanche ukiwasili katika Makaburi ya Waislamu Nguzonane Manispaa ya Shinyanga kwa ajili ya mazishi.
Mamia ya wananchi wa Shinyanga wakiwa kwenye Makaburi ya Waislamu Nguzonane kwa ajili ya kuuzika Mwili wa Marehemu Rajabu Masanche.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu akishiriki mazishi ya Rajabu Masanche.
Mwili wa Marehemu Rajabu Masanche ukipumzishwa kwenye makazi yake ya milele.
Mwili wa Marehemu Rajabu Masanche ukipumzishwa kwenye mkazi yake ya milele.
Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, (kulia) ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye ulemavu akishiriki mazishi ya Rajabu Masanche.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم