WATUHUMIWA 15 WADAKWA MAUAJI YA WAFUGAJI TUNDURU


Mifugo iliyokamatwa na kikosi maalum cha Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi kupitia kikosi cha kupambana na kuzuia wizi wa mifugo Nchini limesema linawashikilia watuhumiwa 15 waliohusika katika tukio la mauaji ya wafugaji katika kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma.


Hayo yamesemwa leo Septemba 24 2022 na Kamanda wa Polisi kikosi cha kuzuia wizi wa mifugo na migogoro ya wakulima na wafugaji nchini Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP SIMON PASUA alipofika Kijiji cha Mbatamila wilaya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo linawashikilia watuhumiwa kumi na tano (15) kwa kosa la mauaji ya vijana wanne wa familia moja katika Kijiji cha mbatamila nakusema kuwa wale wote waliofanya mauaji hayo hawako salama nakuwataka wajisalimishe Jeshi la Polisi.


Aidha amewataka wakulima na wafugaji kutojichukulia sheria mkononi na badala yake wafuate misingi ya sheria na taratibu katika kutatua Changamoto zilizopo.

Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Simon Pasua akiongea na Wananchi wa Tunduru-Ruvuma

Sambamba na hilo amewapa Pole wananchi waliopoteza ndugu zao ambapo kamanda Pasua amesema Jeshi hilo linaendelea kuwatafuta watuhumiwa wote walio baki ili wafikiahwe katika vyombo sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.



Pia kamanda Pasua amesema kuwa Jeshi hilo limefanikiwa kukamata mifugo 159 iliyokuwa imeibiwa katika Kijiji cha Mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma ambapo amesema Jeshi hilo linaendelea kushrikiana na wafugaji na wakulima katika kupambana nauhalifu wowote ule.
Kwa upande wake katibu wa chama cha wafugaji Nchini Bi. Prisca Kaponda amesema wao kama chama cha wafugaji kitaendelea kutoa elimu kwa wafugaji juu ya matumizi bora ya ardhi ili kumaliza migogoro ya wakuliama nawafugaji hapa nchini.



Nao baadhi ya wahanga wa tukio hilo wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa jitihada walizo chukua za kuwakamata watuhumiwa wa matukio ya mauaji na kukamata mifugo ilikuwa imeibiwa katika Kijiji cha mbatamila Wilaya ya Tunduru Mkoa wa Ruvuma na kuliomba Jeshi hilo kuweka nguvu kubwa ili kupata mifugo ambayo haijapatikana.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments