RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI MUDA HUU


********************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

Amemteua Bw. Peter Ilomo kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF). Bw. Ilomo ni Katibu Mkuu Mstaafu. Bw. Ilomo anachuka nafasi ya Dkt. Moses M. Kusiluka ambaye amemaliza kipindi chake.

Amemteua Bi. Mwantumu Bakari Mahiza kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali. Bi. Mahiza ni Skauti Mkuu Tanzania.

Uteuzi huu unaanza mara moja

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments