UGONJWA WA AJABU WAIKUMBA FAMILIA NZIMA


Helena Hungoli

MKAZI wa kijiji cha Imbilili Juu kilichopo Wilaya ya Babati, mkoani Manyara amezungumzia maumivu anayopata kutokana na ugonjwa wa ngozi kuning’inia na kufunika uso na mdomo.


Familia moja huko katika Wilaya ya Babati mkoani Manyara iliyopo katika kijiji cha Imbilili Juu, imekumbwa na ugonjwa wa ajabu baada ya watu wa familia hiyo ambao ni Helena Hungoli mwenye umri wa miaka 60 anayeishi na ndugu zake wengine kukumbwa na ugonjwa wa ajabu wa ngozi kuning’inia na kufunika pua na mdomo.


Pia katika familia hiyo wapo watoto wawili ambao ni watoto wake na Helena Hungoli, pamoja na ndugu zake ambao wote wanaishi kwenye kibanda kidogo wameugua ugonjwa huo.


Helena ameiomba Serikali na wasamaria wema kumsaidia, kwa kumuwezesha kutibu tatizo la ugonjwa huo ambao amedumu nao kwa zaidi ya miaka 55.


Wakati akizungumza amesema kwa sauti ya chini yenye majonzi:


“Kila sehemu ya mwili wangu inauma na kwa hali niliyo nayo, inanibidi nishinde nyumbani muda wote na sasa nahitaji msaada mkubwa, Serikali na wasamaria wema nisaidieni”


Kwa sasa amesema hawezi kufanya kazi yoyote ya kumuingizia kipato, kutokana na kuwa na hali ya ugonjwa huo tangu akiwa mdogo hadi sasa, hivyo ameiomba Serikali na wasamaria wema kuweza kumsaidia yeye pamoja na familia yake kuondokana na tatizo la ugonjwa huo.

Chanzo - Global Publishers

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments