MWALIMU MKUU AFARIKI AKIAMUA UGOMVI WA JIRANI YAKE




Mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni Moi Buruma
**
MWALIMU Mkuu wa Shule Ya Msingi Taisi iliyopo kata ya Burmea mkoani Mara, Ibrahimu Maryoba ameaga dunia kutokana na ugonjwa wa shinikizo la damu wakati akienda kuamua ugomvi wa jirani yake.


Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa kijiji cha Sokoni, Moi Buruma aliyesema kuwa mwalimu huyo mauti yalimukuta wakati akiwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Nyairoma alipokwenda kuamulia ugomvi wa jirani yake Juma pamoja na mkewe baada ya kusikia kelele za kuomba msaada zilizopigwa na mke wa bwana huyo.

Mwalimu huyo baada ya kutoka nje alianguka na kupoteza fahamu ambapo wasamaria wema walifika na kumpeleka Kituo cha Afya cha Sirari, lakini alifariki dunia akiwa bado anapatiwa huduma.


Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarikikya amethibitisha kutokea kwa kifo hicho ambacho kilitokana na shinikizo la damu kulingana na maalezo ya daktari wa hospitali alipofia marehemu pia amewataka wananchi kuwa watulivu na kuacha kueneza habari zisizo nauhakika.

Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Tarime Rorya ACP Geofrey Sarikikya

“Tunaendelea na uchunguzi zaidi na tunawaomba wananchi kuwa watulivu na kuacha kueneza mambo yasiyo na uhakika na badala yake wafuate mambo ya kitaalamu kama ilvyoelezwa na daktari kwamba marehemu amefariki kutokana na shinikizo la damu” alisema kamanda huyo.


Mwili wa marehemu ulipelekwa hospitali ya wilaya ya Tarime kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi na ulirejeshwa nyumbani kwake katika kitongoji cha Nyairoma kwa ajili ya taratibu za mazishi.

Imeandikwa na: Oswald Mwesiga wa msaada wa mitandao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments