MWANAMKE AJIUA KWA KITENGE CHUMBANI


Elizabeth Cheleo mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa mtaa wa Nsemulwa, Kata ya Nsemulwa wilaya ya Mpanda mkoani Katavi, amepoteza maisha kwa kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia kipande cha kitenge alichokining'iniza juu ya kenchi.


Taarifa hiyo imetolewa na Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Ali Makame Hamad, na kusema kwamba baada ya uchunguzi jeshi hilo lilibaini kwamba marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa akili.

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments