RAIS SAMIA AHESABIWA IKULU ..."NIITAKIE NCHI YETU SENSA NJEMA"


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza na Karani wa Sensa Phausta Ntigiti wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
 ****
RAIS Samia leo Jumanne, Agosti 23, 2022 amekuwa miongoni mwa Watanzania waliohesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza saa 6:01 usiku.


Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Albina Chuwa na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022, Anne Makinda wameongoza timu kwenda Ikulu ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kumhesabu Rais Samia.


Mara baada ya kumaliza kumhesabu, kazi iliyodumu si zaidi ya nusu saa, Rais Samia amezungumza na waandishi wa habari akisema, “Nimemaliza kuhesabiwa, ni kweli maswali ni mengi kidogo lakini yanajibika, ombi langu kwa wananchi ni kuweka taarifa zetu mapema.”


Rais Samia amemaliza kuzungumza kwa kusema, “Niitakie nchi yetu sensa njema, makarani wetu wafanye kazi kwa ufanisi na wananchi wajitokeze kutoa majawabu yanayotakiwa.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments