AJALI YAUA 19 , KUJERUHI 10 MBEYA

Idadi ya watu waliofariki katika ajali iliyotokea  leo Agosti 16, 2022, katika eneo la mteremko wa Inyala Pipeline wilayani Mbeya imefikia 19 ambapo kati yao wanaume ni 12 wanawake sita na mtoto mmoja.

Aidha watu 10 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo ambapo wanaendelea kupata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya na Igawilo. Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Ulrich Matei amethibitisha usiku huu.

Ajali hiyo imetokea hii leo majira ya saa 2:00 asubuhi, huku chanzo cha ajali kikielezwa kuwa ni kufeli kwa breki ya lori iliyopelekea lori hilo kuparamia magari mengine yaliyokuwa chini ya mlima.
Ni kwamba mnamo tarehe 16.08.2022 majira ya saa 02:00 asubuhi huko maeneo ya Inyala Pipeline, Kijiji cha Shamwengo, Kata ya Inyala, Tarafa ya Tembela, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya katika barabara ya Mbeya – Njombe, Gari lori lenye namba za usajili T.387 DFJ lenye tela namba T.918 DFE aina ya Dayun likiendeshwa na Dereva MUHSIN GUMBO, Mkazi wa Dar es Salaam mali ya kampuni ya Evarest Frech Ltd likiwa na kontena la mchanga likitokea Mbeya liligonga kwa nyuma Gari T.966 DUQ aina ya Fuso basi mali ya kampuni ya Super Rojas likitokea Mbeya kuelekea Njombe likiendeshwa na ALEX MGIMBA [51] Mkazi wa Jijini Mbeya na kisha kugonga Gari T.836 DRE Mitsubish Benz iliyokuwa ikiendeshwa na NEDIM PREMJI, Mkazi wa Dar es Salaam na kisha kugonga Gari linguine T.342 CHG/T.989 CGS Scania iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika na kusababisha vifo vya watu 19 kati yao wanaume ni 12, wanawake 06 na mtoto 01. Aidha katika ajali hiyo majeruhi ni 10 kati yao wanaume ni 07, wanawake ni 02 na mtoto 01.


Chanzo cha ajali ni Gari kufeli breki kwenye eneo lenye mteremko mkali na kisha kugonga magari mengine. Miili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Rufaa Mbeya na Hospitali ya Igawilo.


Imetolewa na:
Ulrich Matei – SACP
Kamanda wa Polisi,
Mkoa wa Mbeya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments