AKAMATWA AKIJARIBU KUMTAPELI MKURUGENZI WA HALMASHAURI AKIJIITA MKUU WA IDARA YA USALAMA WA TAIFA


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi Ally Hamad Makame.

Na Walter Mguluchuma -Malunde 1 blog Katavi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi limemkamata Raymond Njofu Bwire(28) Mkazi wa Kamguluki Mkoa wa Mara kwa tuhuma za kumtumia ujumbe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlele Mkoani Katavi Teresia Irafy kwenye simu yake ya mkononi  ukieleza amsaidie nafasi ya kupata kazi ya mtu mmoja ya utendaji wa Kijiji na kujitambulisha kwa jina la Diwani Athumani Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi All Hamad Makame amesema mtuhumiwa huyo alifanya tendo hilo hapo Julai 17 mwaka huu kwa kutumia simu yake ya mkononi .


Amebainisha kuwa baada ya ujumbe kuwa umepokekewa na taarifa kutolewa kwa vyombo vya usalama uchunguzi ulianza mara moja kwa ushirikiano wa vyombo vya usalama katika Mkoa wa Katavi na nje ya Mkoa wa Katavi.

Kamanda All Hamad Makame ameeleza kuwa kufuatia uchunguzi huo uliofanywa na vyombo vya ulinzi na usalama na ilipofika mnamo tarehe nane mwezi huu wa Agosti waliweza kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa Raymond Njofu Bwire katika Kijiji cha Kamguluki huko Mkoani Mara.

Alisema kuwa baada ya mtuhumiwa kuwa amekamatwa alifanyiwa mahojiano na jeshi la Polisi na katika mahojiano hayo amekiri kuwa ni yeye aliyetuma ujembe huo wa maandishi kwa njia ya simu yake ya mkononi na kujifanya kuwa ni Diwani Athumani Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.


Mtumiwa huyo tayari amesafirishwa kutoka Mkoani Mara na sasa yupo Mkoani Katavi akiwa anaendelea kushikiliwa na jeshi la polisi kwa mAhojiano na anatarajiwa kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments