WAANDISHI WA HABARI WANAWAKE WAPATIWA MAFUNZO YA UANDISHI WA HABARI ZA UCHUNGUZI

Mkuu wa wilaya Kigoma Ester Mahawe akizungumza wakati wa kufunga mafunzo ya siku nne ya uandishi wa habari za uchunguzi kwa waandishi wa habari wanawake yaliyofanyika mkoani Kigoma. (Picha na Fadhili Abdallah).Mwandishi w habari wa Chanel Ten ambaye pia ni Katibu wa Chama cha waandishi wa habari mkoa Kigoma Mwajabu Kigaza (kulia) akipokea cheti cha kuhitimu mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyowashirikisha waandishi wa habari wanawake kutoa mikoa mbalimbali ya Tanzania kwa uratibu wa baraza la habari Tanzania )MCT).
Mkuu wa wilaya Kigoma Ester Mahawe (wa pili kushoto) akikabidhi kwa Mwandishi wa habari Stella Ibengwe cheti cha kuhitimu mafunzo ya siku nne ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyofanyika mkoani Kigoma mwishoni mwa wiki kwa uratibu wa baraza la habari nchini (MCT).
Mwandishi wa habari wa ITV mkoa Mara Jackline Masinde (kulia) akipokea cheti baada ya kuhitimishwa kwa mafunzo ya siku nne ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyofanyika Kigoma kwa uratibu wa baraza la habari nchini (MCT) ambapo waandishi wa habari 17 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania walishiriki.
Waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambao walishiriki mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi yaliyofanyika mkoani Kigoma kwa uratibu wa Baraza la habari Tanzania (MCT) . (Picha na Fadhili Abdallah)

Na Fadhili Abdallah,Kigoma


WAANDISHI wa habari nchini wameaswa kutumia mafunzo ya umahiri wa uandishi wa habari wanayoyapa kuleta mchango wa maendeleo na ustawi bora kwa taifa badala ya kutumia mafunzo hayo kuigombanisha serikali na wananchi wake.

Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema hayo akifunga mafunzo ya siku nne ya uandishi wa habari za uchunguzi wa kina kwa waandishi wa habari wanawake yaliyofanyika mkoani Kigoma kwa uratibu wa Baraza la habari Tanzania (MCT).

Katika hotuba iliyotolewa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya Kigoma,Ester Mahawe alisema kuwa uandishi wa habari za uchunguzi unaozingatia uzalendo na maadili ya taaluma hiyo una manufaa makubwa kwa maendeleo ya taifa na ustawi kwa watu wake lakini kinyume chake uandishi wa habari za uchunguzi umesababisha taharuki kubwa kwa nchi na viongozi wake.

“Nawapongeza waandishi wa habari wanawake kutoka mikoa yote waliohudhuria mafunzo haya, yawajenga kuwa mahiri katika kufanya uchunguzi wa kina lakini unaozingatia taaluma, msingi wa maendeleo ya nchi na usioleta uchochezi au kuigombanisha serikali na wananchi wake,”alisema Andengenye.

Awali Katibu Mtendaji wa Baraza la habari nchini (MCT),Kajubi Diocles Mukajanga alisema kuwa mafunzo hayo ya siku nne kwa waandishi wa habari wanawake 17 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania bara yamelenga kujenga uwezo kwa waandishi hao kufanya stori na makala ambazo zinaelezwa kuwa haziwezi kufanywa na wanawake.

Alisema kuwa chini ya Mkufunzi wa mafunzo hayo, Laurence Kilimwiko waandishi wa habari hao wanawake wanajengewa uwezo wa kuibua na kwenda kufanya habari na makala zilizofanyiwa uchunguzi wa kina kuondokana na habari za uchungizi wa kawaida.

Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Harieth Makweta kutoka gazeti la Mwananchi Dar es salaam akizungumza baada ya mkuu wa wilaya Kigoma,Ester Mahawe kuyafunga rasmi alisema kuwa mafunzo hayo yamekuwa nyenzo kubwa kwao katika kuboresha utendaji kazi wao katika kuandika habari za uchunguzi.

Makweta alisema kuwa katika mafunzo hayo walijifunza namna ya kuandika habari za uchunguzi hasa kuondokana na dhana za habari za uchunguzi ambazo ndani yake hakuna jambo kubwa la ziada ambalo mwandishi amelifanya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments