TANESCO YAAHIRISHA MPANGO WA KUZIMA MFUMO WA UNUNUZI LUKU





Awali Tanesco ilitangaza kuwa Wananchi hawataweza kununua umeme kwa njia ya Luku kwa siku nne, Agosti 22 - 25, 2022 kuanzia saa 4 usiku hadi saa 1 asubuhi kutokana na matengenezo kwenye kanzidata ya mfumo wa Luku.


Mapema leo Meneja Mwandamizi wa Tehama katika Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Cliff Maregeli alisema matengenezo hayo yanalenga kuongeza ufanisi katika mfumo wa Luku huku akiwataka wananchi kununua umeme wa kutosha katika kipindi hiki kwa sababu hawataweza kununua umeme wa Luku katika kipindi kilichobainishwa.

"Wananchi wazingatie tu kununua umeme wa kutosha ili waepuke usumbufu unaoweza kujitokeza," alisisitiza Msemaji wa Tanesco, Martin Mwambene.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments