WAZIRI MHAGAMA ATIMIZA AHADI YA KUWASHA UMEME NAKAWALE... WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI

Mbunge wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utawala bora akisalimiana na wananchi

Na  Andrew Chatwanga - Songea

Wananchi wa Kijiji cha Nakawale kata ya Mhukuru wilaya ya Songea Mkoa wa Ruvuma (Jimbo la Peramiho) wamemshuru Mbunge wao wa jimbo la Peramiho Jenista Mhagama ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais utawala bora kwa kutimiza ahadi ya kuwapatia umeme licha  kijiji hicho kuwa mpakani mwa nchi jirani ya Msumbiji.

Wakiongea kwa Nyakati tofauti na Mwandishi wa habari hizi walisema walikata tamaa kwa vile Kijiji hicho kipo mbali na makao makuu ya wilaya na kipo mpakani wakitenganishwa na mto Ruvuma lakini sasa Umeme umewashwa rasmi na kuzinduliwa na Jenista Mhagama mbunge wao.

Akizindua umeme huo Mheshimiwa Jenista Mhagama,alimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kukubali kutoa fedha ambazo zimesaidia kufanikisha mradi na sasa alicho wahaidi wananchi wa Kijiji hicho na vijiji vingine vinavyopitia mradi huo umeme umewaka na kuwataka wananchi kuendelea na kazi zao za uzalishaji mali kupitia kilimo na yeye muda wote atakuwa nao kuhakikisha wanapa maendeleo.

Mhe. Mhagama alisema umeme ni fursa ya maendeleo na kubadilisha mitazamo ya wananchi na mpakani hapo wamejenga soko kubwa la kimataifa la mazao ambayo sasa kwa kuwa na umeme itasaidia sasa kukamilika kwa mradi wa maji ambao Shirika la Masista la Chipole wameanza kusambaza maji kwenye maeneo yao.


Mhandisi Mkuu wa Tanesco Mkoa wa Ruvuma Hamis Sosthenes aliyesimamia mradi huo alisema jimbo la Peramiho lina jumla ya Vijiji 56 kati ya hivyo vjiji 32 vimeshapatiwa umeme vimewashwa nab ado vijiji 24 ambavyo viko kwenye mpango wa REA awamu ya tatu mkandarasi yuko kazini anaendea na wao wanamsimamia vizuri ili akamalishe mradi kwa wakati.

             

Mhandisi Sosthenes alitambulisha huduma mpya ambayo sasa itawapunguzia adha wanachi ya kusafiri umbali mrefu ili kupata huduma ya kuunganishiwa umeme na sasa watatumia NIKONEKT ambayo wanaomba kuunganishiwa umeme kupitia simu ,kwa kutumia huduma hiyo umem unaunganishwa kwa siku nne tu .

 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments