RAIS SAMIA AKUTANA NA KUZUNGUMZA MAKAMU WA RAIS WA MAREKANI , IKULU YA MAREKANI JIJINI WASHINGTON


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya kuwasili Ofisini kwake katika Ikulu ya Marekani White House Washington leo tarehe 15 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris wakati wakizungumza na Wanahabari katika Ikulu ya Marekani White House Washington leo tarehe 15 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris wakati akiangalia mandhari ya Majengo ya Ofisi za Ikulu ya Marekani mara baada ya kuzungumza na Wanahabari katika Ikulu hiyo ya White House Washington leo tarehe 15 Aprili, 2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mazungumzo Rasmi na Ujumbe wa Serikali ya Marekani ulioongozwa na Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris katika Ikulu ya White House Washington leo tarehe 15 Aprili, 2022.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Makamu wa Rais wa Marekani Mhe. Kamala Harris mara baada ya mazungumzo na Ujumbe wa Tanzania katika Ikulu ya Marekani Whitehouse nchini Marekani leo tarehe 15 Aprili, 2022. PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments