STAA WA FILAMU UKRAINE AUAWA VITANI



Staa mkubwa wa filamu nchini Ukraine, Pasha Lee aliyeamua kuweka sanaa pembeni na kuingia vitani kuipigania nchi yake, ameuawa baada ya kupigwa na makombora ya Urusi katika Mji wa Irpin ambako mashambulizi makali yanaendelea.

Pasha aliyefariki akiwa na umri wa miaka 33, alipata umaarufu mkubwa kutokana na kazi yake ya uigizaji na utangazaji ambapo filamu za Lion King na Hobbit, zilimfanya apate umaarufu ndani na nje ya nchi hiyo.

Siku tano kabla ya mauti yake, staa huyo ambaye ni mzaliwa wa Crimea, aliposti picha katika mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa amevaa mavazi ya kijeshi na kusindikiza na maneno ya ‘LET’S UNITE’ akiwataka wananchi wa Ukraine kuungana kupambana na uvamizi wa Urusi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments