AFISA WA AFYA SHIRIKISHO LA SOKA AFRIKA CAF AFARIKI DUNIA


Dr Joseph Kabungo enzi za uhai wake

**

Afisa wa afya wa shirikisho la soka Afrika CAF, Dr Joseph Kabungo amefariki dunia baada ya kupatwa na shambulio la moyo baada ya kumalizika kwa mchezo baina ya Ghana dhidi ya Nigeria na mashabiki kuingia uwanjani kwenye dimba la Abuja International Stadium

Dr Kabungo ambaye alikuwa msimamizi wa mchezo huo kwenye idara ya afya kutokea CAF, taarifa za awali zinasema alipatwa na umauti kutokana na ugonjwa wa shambulio la moyo pindi mashabiki walipoingia uwanjani baada ya mchezo kumalizika dakika 90 huku shirikisho la soka la Zambia likitoa taarifa kusubiri ripoti kamili kutoka CAF na FIFA juu ya chanzo cha kifo cha daktari huyo .

“Ni mapema kusema chanzo kilichosababisha kifo cha Dr Kabungo lakini tunasubiri ripoti kamili kutoka CAF na FIFA kuhusu undani wa tukio hilo” amesema Rais FAZ Andrew Kamanga kupitia mtandao wa Twitter

Enzi za uhai wake alidumu kama daktari wa timu ya taifa ya Zambia “Chipolopolo” kuanzia mwaka 2003 mpaka 2016 huku siku za karibuni alichaguliwa kuwa katika kamati ya matabibu ya FIFA baada ya hapo awali kuwa mjumbe wa kamati ya matabibu wa CAF.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments