IGP SIRRO AFANYA MABADILIKO YA MAKAMANDA WA POLISI..RPC ALIYETAKA KUWA IGP ARUDISHWA MAKAO MAKUU


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amefanya uhamisho wa mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Polisi wa Mikoa.


Katika uhamisho huo, aliyekuwa RPC Mkoa wa Kagera, ACP Wankyo Nyigesa amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake inachukuliwa na aliyekuwa RPC Rukwa, ACP William Mwampagale. 


Kwa mujibu wa taarifa ya Jeshi la Polisi iliyotolewa leo Jumanne Machi 29, 2022 uhamisho huo umefanyika ili kupisha uchunguzi wa tukio la tarehe 26.3.2022 katika sherehe ya kumuaga aliyekuwa RPC mkoa wa Pwani ambapo ACP Wankyo alitoa maneno ambayo yanaonyesha kuwepo na ukiukwaji wa nidhamu kulingana na miongozo ya Jeshi la Polisi.


Taarifa hiyo haijasema maneno hayo, ila hivi karibuni alinukuliwa akiomba kuteuliwa na Rais kuwa IGP baada ya kukosa nafasi za DCI na Kamishna Zanzibar.


Pia katika mabadiliko hayo, Aliyekuwa Afisa Mnadhimu Mkoa wa Rukwa, ACP Theopista Mallya anakuwa RPC wa mkoani Rukwa aliyekuwa Mkuu wa Operesheni Rukwa, ACP Mashenene Mayila anakuwa Afisa Mnadhimu wa mkoa huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments