YANGA SC YAENDELEA KUTAKATA, YAICHAPA KAGERA SUGAR 3-0
****************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM


KLABU ya Yanga imeendelea kujichimbia kileleni mara baada ya kufanikiwa kuichapa Kagera Sugar mabao 3-0 wenye dimba la Benjamini mkapa Jijini Dar es Salaam.

Fiston Mayele amekuwa akizidi kuwa bora kila kukicha mara baada ya leo kufanikiwa kupachika mabao mawili kwenye mchezo wa leo na kufikisha mabao tisa kwenye ligi ya NBC.

Mayele alianza kupata bao la maepma zaidi na kuisaidia timu yake iongozi mapema tu kabla ya baadae kupachika bao la pili akipokea pasi kutoka kwa Said Ntibazokiza.

Saidi Ntibazokiza nae hakuwa nyuma kwenye mchezo wa leo ambapo ametengeneza mabao mawili na lingine akipachika mwenyewe.Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم