SIMBA SC YAUWASHA MOTO, YAICHAPA DAR CITY MABAO 6-0



***************

EMMANUEL MBATILO,DAR ES SALAAM

KLABU ya Simba imefanikiwa kusonga mbele kombe la Azam Federation Cup mara baada ya kufanikiwa kuwachapa mvua ya magoli timu ya Dar City mabao 6-0.

Simba imeingia hatua hiyo magoli yakiwekwa kimyani na Meddie Kagere ambaye amefunga mabao 2 na mengine yakifungwa na Chama, Bwalya,beki wao kisiki Wawa na Chri Mugalu ambaye alifunga mahesabu ya mabao katika uwanja huo wa Benjamini mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba sc imewachukua mechi nne kupata ushindi kwa mara ya kwanza hivyo nakuwaacha mahasimu wao Yanga kuendelea kushika usukani wa ligi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments