KUELEKEA USIKU WA UZINDUZI WA TUZO ZA MUZIKI


****************

Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt Hassan Abbasi amesema Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) inakwenda kuweka wazi vigezo vya tuzo za muziki ili wasanii waweze kushiriki kikamilifu na kushinda tuzo za miziki ambazo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imefufua sasa baada ya miaka saba kupita bila tuzo hizo.

Dkt. Abbasi amesema hayo leo alasiri Januari 28, 2022 kwenye kipindi cha XXXL kilichorushwa mbashara kuhusu Uzinduzi wa Tuzo za Muziki na Ugawaji wa mirabaha kwa wasanii unaofanyika usiku wa leo Januari 28,2022 kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ni Waziri mwenye dhamana ya Sanaa nchini Mohamed Mchengerwa ambapo wadau mbalimbali wa Sanaa na vikundi mbalimbali vya wasanii vimealikwa kutumbuiza kwenye hafla hii inayokwenda kwa jina la#2 KUBWA ZA2022.

Ameongeza kuwa baada ya kuweka wazi vigezo hivyo mtandaoni zitafuata warsha za uelimishaji kwa wasanii.

Amesema kilele cha utoaji wa tuzo hizo utakuwa Machi 26, 2022 ambapo ametaja baadhi ya vigezo vya jumla vya kuzingatia ni kuwa washiriki lazima wawe watanzania.

Vigezo vingine ni lazima kuthibitisha umiliki wa kazi hiyo na kazi hiyo iwe imetoka ndani ya kipindi cha mwaka 2021.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments