RAIS SAMIA : TUTAENDELEA KUKOPA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
**
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amesema kwamba serikali yake itaendelea kukopa kwa lengo la kumaliza na kuikamilisha miradi yote ya maendeleo.

Kauli hiyo ameitoa hii leo Desemba 28, 2021, jijini Dar es Salaam, mara baada ya kushuhudia hafla ya utiaji saini mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) awamu ya tatu kipande cha Makutupora hadi Tabora.

Rais Samia amesema serikali itaendelea kuchukua mikopo nafuu kutoka kwa nchi wahisani, ili kukamilisha mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ambao mpaka sasa gharama za ujenzi wake zimefikia shilingi trilioni 14.

Amesema tayari ameiagiza wizara ya ujenzi na uchukuzi kukamilisha utaratibu wa manunuzi ili kumpata mkandarasi wa reli ya Tabora- Isaka na Tabora- Kigoma na baadaye Kaliua-Mpanda mpaka Kalema.

“Leo hii tumekusanyika hapa kushuhudia utiaji saini mkataba wa ujenzi wa reli ya kisasa kwa kipande cha kutoka Makutupora hadi Tabora, KM 368 na mkataba huu una thamani ya Tsh trilioni 4.41 ukijumuisha na kodi ya ongezeko la thamani.

“Uwekezaji mpaka sasa hivi ni Tsh tril 14.7 tusipoendelea na ujenzi wa reli tukakamilisha fedha hizi tulizozilaza chini zitakuwa hazina maana kwa njia yoyote tutakopa sababu fedha hizi hatutazitoa kwenye tozo, wala kodi tunazokusanya ndani",amesema

Kazi ya ujenzi wa Reli ya Kisasa ni kazi kubwa yenye kuhitaji uthubutu mkubwa wa Serikali na wananchi, nitumie fursa hii kuwapongeza Watanzania wote kwa mafanikio haya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments