MWANAMKE MWINGINE AUAWA JIJINI ARUSHA


Happy Lazaro, Arusha
Mwanamke mwingine mkazi wa Njiro, jijini Arusha,Janerose Dewasi(66) ameuawa kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali na anayetuhumiwa ni mfanyakazi wake wa ndani.


Tukio hili  limetokea siku chache baada ya mwanamke mwingine,Ruth  Mmasi kubainika kuuawa eneo la Njiro pia na anayetuhumiwa ni mtoto wake wa kiume Patrick Mmasi(19)


Kamanda wa  polisi mkoani Arusha,Justine Masejo amethibitisha kutokea mauwaji hayo kubainika leo saa 2:30 asubuhi na kueleza kuwa polisi  wanamsaka  mfanyakazi wa ndani ambaye anatuhumiwa baada ya kufanya mauaji hayo alitoweka.


Kamanda Masejo amesema imebainika mwanamke huyo ambaye alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo kwenye nyumba yake eneo la block D mwili wake umepigwa na kitu chenye ncha kali kwenye paji la uso kushoto.


"Uchunguzi wa awali umebaini kuwa marehemu alikuwa anaishi na mfanyakazi huyo wao pekee na alimuajiri wiki moja iliyopita”amesema


Hata hivyo amesema mara baada ya mauwaji hayo mfanyakazi huyo ametoweka na anaendelea kusakwa.
Kamanda amesema jeshi la polisi linatoa wito kwa wenye nyumba kuwa makini na wafanyakazi wa ndani wanaowapa kazi kwa kujua historia zao.


Mmoja wa majirani wa nyumba hiyo,Mary Muchi alisema mfanyakazi huyo alikuwa hajulikani sana mtaani kwani ameanza kazi muda si mrefu.


“Hatujui lolote huyo kijana anatajwa Boniface alikuwa akiimsaidia huyu mama kazi zao na leo tumeshangaa kupata taarifa za kifo cha mama huyu”,amesema.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments