Mashirika Ya Kigeni Yazidi Kuvutiwa Kuwekeza Katika Sekta Ya Nishati Tanzania
الثلاثاء, نوفمبر 30, 2021
Na Dorina G. Makaya - Dar-es-Salaam.
Idadi ya mashirika ya kigeni yanayovutiwa kuwekeza katika sekta ya Nishati nchini yameendelea kuongezeka ikiwemo katika sekta ndogo ya umeme na nishati Jadidifu.
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, tarehe 29 Novemba, 2021, amekutana na Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mitsubishi iliyopo jijini Dar--es-Salaam, Kenji Nishizaki na kujadili masuala ya ushirikiano wa kisekta na fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini Tanzania.
Miongoni mwa masuala waliyoyazungumzia katika mkutano huo, uliofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara ya Nishati, ni pamoja na kupanua wigo wa biashara kwa kutazama fursa zilizopo za uwekezaji katika maeneo ya sekta ndogo ya umeme, mafuta na gesi asilia pamoja na ushirikiano wa kisekta kwa ujumla na Serikali ya Tanzania
Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba, amewakaribisha Kampuni ya Mitsubishi kwa ajili ya kuwekeza hapa nchini na ameelekeza mashirika ya TPDC na TANESCO kutazama kwa upana zaidi wigo huo wa uwekezaji ambao Mitsubishi wanataka kuwekeza.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin