MTOTO WA MIAKA 6 AJIPIGA RISASI GEITA


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe
**
Mtoto wa miaka sita Eric Joshua Mkandi mkazi wa kitongoji cha Mkapa kijiji cha Izumangabo kata ya Bwanga, mwanafunzi wa darasa la kwanza shule ya msingi Izumangabo amefariki dunia kwa kujipiga risasi.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita limesema tukio hilo limetokea November 13,2021 katika Kitongoji cha Mkapa Kijiji cha Izumangambo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Henry Mwaibambe amesema mtoto Eric amefariki dunia wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Bwanga baada ya kujipiga risasi kwa silaha aina ya Pistol Beretta inayomilikiwa na baba yake kwenye paji la uso na kutokea kisogoni akiwa ndani ya chumba cha baba yake mzazi aitwaye Joshua Mkandi.

Kamanda Mwaibambe amesema silaha aliyoitumia Mtoto huyo kujipiga risasi ni aina ya pistol Berreta yenye namba TZS AR74955/E.86808Y ambayo inamilikiwa kihalali na Baba yake Mzazi huku chanzo cha tukio kikiwa ni Mtoto kutokujua madhara yatokanayo na utunzaji mbaya wa silaha hiyo.

“Niwaombe Wamilki wote wa silaha wawe makini katika kutunza silaha zao kwani wanapokuwa wanakabidhiwa wanaelekezwa namna ya kutunza silaha hizo”, amesema Kamanda Mwaibambe

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
أحدث أقدم